China yatoa wito wa kuungana mkono kithabiti kati ya China na Afrika na kuwa na ushirikiano wa kimkakati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akihudhuria na kuhutubia tafrija ya kuadhimisha Siku ya Afrika iliyofanyika Beijing, China, Mei 25, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akihudhuria na kuhutubia tafrija ya kuadhimisha Siku ya Afrika iliyofanyika Beijing, China, Mei 25, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amehudhuria tafrija ya kuadhimisha Siku ya Afrika siku ya Alhamisi mjini Beijing, na kutoa mapendekezo ya kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika.

Akihutubia katika hafla hiyo, Qin kwa niaba ya serikali ya China ameupongeza Umoja wa Nchi Huru za Afrika kwa kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, akibainisha kuwa Afrika imekuwa nguvu muhimu yenye ushawishi wa kimataifa na hadhi ya kimataifa inayopanda.

“Kuingia katika zama mpya ya kujenga jumuiya iliyo karibu zaidi kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, China na Afrika zinahitaji kuimarisha umoja na ushirikiano zaidi kuliko hapo awali,” Qin amesema.

Ametoa wito kwa China na Afrika kulinda kithabiti haki na maslahi halali ya kila mmoja wao na kuimarisha zaidi uungaji mkono wa pande zote katika masuala yanayohusu mamlaka, maendeleo na heshima ya kila mmoja wao.

China na Afrika zinapaswa kuhimiza kikamilifu programu za maendeleo ya kisasa zenye sifa bainifu, Qin amesema, akitoa wito kwa pande zote mbili kuhimiza uoanishaji kati ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika na mikakati mingine ya maendeleo ya nchi za Afrika, na kuisaidia Afrika kuharakisha ukuaji wa viwanda, ujanibishaji na mseto wa kiuchumi.

Qin amesema China na Afrika zinapaswa kuhimiza kwa pamoja mageuzi ya mfumo wa utawala wa kimataifa, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea na kuendelea kuunganisha nguvu za nchi zinazoendelea.

Ametoa wito wa kuimarishwa zaidi kwa mabadilishano na kujifunza kwa kila mmoja miongoni mwa ustaarabu na kuharakisha utekelezaji wa Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia barani Afrika.

Demeke Mekonnen Hassen, Naibu Waziri ambaye pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, na Christophe Lutundula, Makamu wa Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walihudhuria tafrija hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha