Wajasiriamali wa Afrika washirikiana na China kwa ajili ya mafanikio na ukuaji kibiashara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2023

Wajasiriamali wakibadilishana maoni kuhusu biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka kwenye Eneo la Biashara Huria la Kimataifa la Djibouti Septemba 2022. [Picha/Xinhua]

Wajasiriamali wakibadilishana maoni kuhusu biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka kwenye Eneo la Biashara Huria la Kimataifa la Djibouti Septemba 2022. [Picha/Xinhua]

Silas Musyoka, anayeishi katika nchi yake ya Kenya, amekuwa akifanya kazi akiwa meneja wa ukuaji wa mauzo katika kampuni ya biashara ya mtandaoni ya Kilimall ya China kwa miaka mitano.

"Bado najifunza kuhusu sekta ya biashara ya mtandaoni inayokua kila mara katika nchi hii. Ninaamini kwamba Kilimall itakuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi nyingi barani Afrika," amesema Musyoka mwenye umri wa miaka 32, ambaye alipata shahada yake ya uzamili katika sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Jinan kilichoko Mji wa Guangzhou katika Mkoa wa Guangdong wa China.

Kilimall ni duka kubwa la manunuzi ya mtandaoni nchini Kenya. Lilianzishwa Mwaka 2014 likiwa na kauli mbiu ya "Kuboresha Maisha kwa Afrika", na ina watumiaji zaidi ya milioni 10 waliojiandikisha.

Kampuni hiyo ni miongoni mwa kampuni nyingine za biashara ya mtandaoni zinazowekeza kwenye fursa za kibiashara zinazoleta matumaini kati ya China na nchi za Afrika.

Musyoka anasema Kilimall imemsaidia kuelewa vyema mienendo ya soko na ugavi katika nchi yake na kile kinachohitajika ili kufanikiwa katika tasnia ya teknolojia ambayo bado iko changa nchini Kenya. Amesema ameshuhudia jinsi biashara ya mtandaoni inavyoboresha biashara za wenyeji.

"Maisha nchini China ni ya haraka, ambapo unapaswa kuendana na hali kwa haraka sana ili kuzoea hali zinazobadilika. Zaidi ya yale yanayofundishwa darasani, uzoefu wako katika masoko, viwanda, maeneo ya kihistoria na ya kitalii na mwingiliano na watu pia huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uzoefu wa kujifunza," amesema.

Musyoka anasema China ina mengi ya kutoa katika masuala ya maarifa, ujuzi na teknolojia.

"Baada ya kujenga kampuni kubwa za biashara ya mtandaoni, China ina ujuzi wa kutusaidia kuwa na uzoefu sawa hapa Afrika," Musyoka amesema.

Wajasiriamali wa Afrika wamekuwa na shauku ya kusafirisha bidhaa zaidi hadi China.

Njagi Kevin Murimi mwenye umri wa miaka 30, ambaye alianzisha Kampuni ya Biashara ya Changsha Connect miaka minne iliyopita, anasema alikuja China kwanza kwa ajili ya ukubwa wa soko.

Murimi anasema idadi ya watu nchini Kenya ni sawa na ile ya Hunan. "China imetoa soko kubwa kwa ajili yangu," amesema.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka jana, mapato kutokana na biashara kati ya China na Afrika yalifikia dola bilioni 137.4, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.6 mwaka hadi mwaka, kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Biashara ya China. Uagizaji kutoka Afrika hadi China ulikuwa dola bilioni 60.6, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.1 mwaka hadi mwaka. Mauzo ya nje kutoka China hadi nchi za Afrika yalikuwa na thamani ya dola bilioni 76.8, ikiwa ni kuongezeka kwa asilimia 14.7 mwaka hadi mwaka.

Mwalimu akimfundisha mwanafunzi wa kigeni kutoka Afrika ujuzi unaohusiana na biashara ya mtandaoni mjini Chongqing, China, Mei 2020. (Picha/China Daily)

Mwalimu akimfundisha mwanafunzi wa kigeni kutoka Afrika ujuzi unaohusiana na biashara ya mtandaoni mjini Chongqing, China, Mei 2020. (Picha/China Daily)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha