Tanzania yasema mipaka yake ni salama, isipokuwa kuna changamoto kwenye mpaka na Msumbiji

(CRI Online) Mei 26, 2023

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa Tanzania Bw. Innocent Bashungwa amesema mipaka ya Tanzania inaendelea kuwa salama licha ya changamoto ndogo ndogo zinazotokea katika baadhi ya sehemu za mipaka.

Akiongea wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwenye bunge la Tanzania, Bw. Bashungwa amesema hali ya usalama katika mpaka wa kati ya Tanzania na Msumbiji ni ya wastani na isiyotabirika kutokana na uwepo wa kundi la kigaidi la Ansar Al Sunna Wal Jammah (AASWJ) lililopo kaskazini mwa Msumbiji, katika maeneo ya mwambao na mpaka mkabala na Mkoa wa Mtwara.

Ametaja changamoto nyingine kuwa ni baadhi ya watanzania kutojua mpaka wa majini kati ya Kenya na Tanzania, na hivyo baadhi ya wavuvi huenda kuvua samaki nchini Kenya na kujikuta wakikamatwa na mamlaka za huko.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha