Zambia yafunga mpaka wake na Tanzania na kuathiri wafanyabiashara wa Tanzania

(CRI Online) Mei 26, 2023

Watanzania wanaofanya biashara ya mazao ya nafaka na nchi jirani ya Zambia, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya Mamlaka nchini Zambia kuzuia shehena za mazao yao na hivyo kuzusha hofu ya kuathiri mitaji yao, kufuatia serikali hiyo kufunga mpaka ikiwa ni njia ya kujihami na baa la njaa.

Imefahamika kuwa mwaka jana serikali ya Zambia ilinunua shehena ya mahindi kutoka kwa wakulima wake ili kukidhi mahitaji ya wananchi wake katika siku zijazo.

Kufuatia hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya biashara zao, Mkuu wa Mkoa wa Songwe nchini Tanzania, Dkt Francis Michael amekutana na kuzungumza na wafanyabiashara hao mjini Tunduma, ambapo amewataka kuwa watulivu wakati Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Serikali ya Zambia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha