IGAD yasema Pembe ya Afrika itakabiliwa na ukame kuanzia mwezi Juni hadi Septemba

(CRI Online) Mei 26, 2023

Jumuiya ya kiserikali ya maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki(IGAD), imesema ukame utashuhudiwa katika eneo kubwa la Pembe ya Afrika kuanzia mwezi Juni hadi Septemba, pamoja na hatari ya kuzidisha hali mbaya ya usalama wa chakula.

Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na Matumizi cha IGAD (ICPAC), chenye makao yake mjini Nairobi, kimesema Djibouti, Eritrea, maeneo ya kati na kaskazini mwa Ethiopia, kaskazini mwa Uganda, na sehemu kubwa za Sudan Kusini na Sudan zitakuwa na mvua kidogo kuanzia Juni hadi Septemba.

Mkurugenzi wa ICPAC Guleid Artan amebainisha kuwa msimu wa mvua wa Juni hadi Septemba huchangia zaidi ya asilimia 50 ya jumla ya mvua kwa mwaka katika eneo kubwa la Pembe ya Afrika, akiongeza kuwa kama hakutakuwa na mvua, hali ya ukosefu wa usalama wa chakula inaweza kutokea.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha