Kenya yafanya shindano la kuongea lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari

(CRI Online) Mei 26, 2023

Shindano la 16 la Daraja la Kuongea Kichina kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari nchini Kenya limefanyika jana alhamisi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta mjini Nairobi.

Shindano hilo linaloandaliwa na Ubalozi wa China nchini Kenya kwa kushirikiana na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Kenyatta na washirika wengine, limefanyika chini ya kaulimbiu ya "Ruka Juu na Kichina".

Wanafunzi wa shule za sekondari nchini Kenya walifanyiwa tathmini katika maeneo matatu, ikiwemo kuongea Kichina fasaha kwa dakika tatu, ufahamu wao juu ya taifa la China, na ufahamu wao wa utamaduni wa Kichina, kama nyimbo za kale na dansi, kaligrafia, michoro na kung-fu.

Mshindi wa shindano hilo alikuwa ni Telema Njoki, aliyeongea kwa ufasaha lugha ya Kichina, ambaye alipata zawadi mbalimbali na pia kupata ufadhili wa kutembelea China baadaye mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha