Nigeria yazindua shirika la ndege la taifa lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2023

Ndege ya shirika jipya la ndege la Nigeria Air,Nigeria Airline ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Abuja, Nigeria, Mei 26, 2023. Serikali ya Nigeria siku ya Ijumaa ilizindua shirika la ndege la Nigeria, Nigeria Air lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu, katika hatua kubwa ya kusonga mbele kwa sekta ya anga katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika. (Picha na Sodiq Adelakun/Xinhua)

Ndege ya shirika jipya la ndege la Nigeria Air,Nigeria Air ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Abuja, Nigeria, Mei 26, 2023. Serikali ya Nigeria siku ya Ijumaa ilizindua shirika la ndege la Nigeria, Nigeria Air lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu, katika hatua kubwa ya kusonga mbele kwa sekta ya anga katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika. (Picha na Sodiq Adelakun/Xinhua)

ABUJA - Serikali ya Nigeria siku ya Ijumaa imezindua shirika la ndege la Nigeria, Nigeria Air lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu, katika hatua kubwa ya kusonga mbele kwa sekta ya anga katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Madhumuni ya kuanzisha shirika la ndege la kitaifa ni kuiweka tena nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika kuwa mhusika mashuhuri katika soko la anga la kimataifa, Waziri wa Usafiri wa Anga wa Nigeria, Hadi Sirika amesema kwenye hafla ya uzinduzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe ulioko mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

"Tuna idadi ya watu. Tuna jiografia. Tuna uchumi. Tuna watu. Tuna ujuzi. Tuna soko," Sirika amesema katika hafla hiyo ambapo alizindua ndege ya Boeing 737-800 ya shirika hilo mbele ya wadau wakuu, wataalamu wa masuala ya anga, na wapenda usafiri wa anga.

Afisa huyo amebainisha kuwa shirika hilo la ndege, linalotarajiwa kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini humo na kuhimiza ukuaji wa uchumi, linawakilisha ushirikiano wa kawaida kati ya sekta ya umma na ya kibinafsi miongoni mwa wafanyabiashara nchini Nigeria, serikali ya Nigeria, na Shirika la Ndege la Ethiopia.

Nigeria na Ethiopia zina idadi ya watu zaidi ya milioni 220 na milioni 120 mtawalia, kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu.

Sirika amesema shirika hilo litaanza safari za nchini Nigeria na kikanda hivi karibuni, na kuongeza kuwa shirika hilo linatarajiwa kutoa nafasi za ajira zaidi ya 70,000 litakapoanza kufanya kazi kikamilifu na kuwa na hadi ndege 30 katika miaka mitano ya kufanya kazi.

Nigeria ilikuwa na shirika la ndege la kitaifa mapema miaka ya 1950, ambalo liliendesha huduma za abiria za kikanda na za nchini. Kutokana na changamoto za kifedha na kiutendaji, shirika hilo lilikoma kufanya kazi Septemba 2012.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha