Kitabu cha "Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya: Maswali na Majibu" Toleo la Kiingereza chatolewa Kuala Lumpur

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2023

Picha hii iliyopigwa Mei 27, 2023 ikionyesha hafla ya kuanza kutolewa kwa Kitabu cha "Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya: Maswali na Majibu" Toleo la Kiingereza, hafla ambayo iliandaaliwa na China  ikiwa nchi mgeni rasmi kwenye Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Vitabu ya Kuala Lumpur huko Malaysia. (Xinhua/Zhu Wei)

KUALA LUMPUR - Hafla ya kuanza kutolewa kwa Kitabu cha "Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya: Maswali na Majibu" Toleo la Kiingereza imefanyika hapa Jumamosi, hafla ambayo imeandaaliwa na China ikiwa nchi mgeni rasmi kwenye Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Vitabu ya Kuala Lumpur huko Malaysia.

Kitabu hiki kinawasilisha ari ya kimsingi, maudhui na mahitaji ya Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya kwa njia ya kina na ya kufikika kirahisi kupitia muundo wa maswali na majibu. Kinaangazia maudhui bora, uwasilishaji wa kiubunifu, vielelezo wazi na lugha iliyo rahisi kueleweka.

Kitabu hicho kimechapishwa kwa ushirikiano na Shirika la Uchapishaji la Xuexi la China na Kampuni ya Vitabu vya GBD ya India, kikilenga nchi zinazozungumza Lugha ya Kiingereza duniani kote. Inasaidia jumuiya ya kimataifa kuelewa kwa kina mawazo muhimu ya Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya, na kuongeza uelewa juu ya hekima na wajibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kilichojitolea kuhimiza ujenzi wa Dunia bora.

Maofisa kutoka Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, watu kutoka sekta za siasa na taaluma, wanahabari na wachapishaji wa Malaysia, na wajumbe kutoka jumuiya ya washauri mabingwa walihudhuria hafla hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha