Viongozi wa Uganda na Tanzania wazindua kituo cha umeme cha kutoa huduma ya kuvuka mipaka

(CRI Online) Mei 29, 2023

Marais wa Uganda na Tanzania wamezindua kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji kinachotoa huduma ya umeme ya kuvuka mipaka ya nchi hizo mbili.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wamezindua kituo hicho chenye kuzalisha umeme wenye nguvu za megawati 16 unaovuka mpaka cha Kikagati-Murongo katika wilaya ya Isingiro, magharibi mwa Uganda.

Rais Museveni amesema umeme wa bei nafuu unahitajika sana haswa kwa shughuli za uzalishaji, na juhudi za kuondokana na umaskini.

Rais Samia amesema kituo hicho kitatoa umeme wa bei nafuu kwa Tanzania, ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuhimiza ushirikiano wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha