Umoja wa Afrika waonya kuwa Afrika haipaswi kuwa "uwanja wa vita vya siasa za kijiografia"

(CRI Online) Mei 29, 2023

Viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) wameonya Afrika haipaswi kuwa "uwanja wa vita vya siasa za kijiografia" kwa nchi zenye nguvu duniani, wakati bara hilo likikabiliana na matishio kadhaa ya amani na usalama wake.

Wakizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuundwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Mei 25, 1963 ambao sasa umebadilishwa jina kuwa Umoja wa Afrika (AU), Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat, amesema katika muktadha huu wa kimataifa wa makabiliano ya maslahi tofauti ya kisiasa, nia ya kila upande inatishia kubadilisha Afrika kuwa uwanja wa vita vya siasa za kijiografia, na hivyo kuleta hali ya vita baridi.

Bara la Afrika limekuwa jukwaa la vita vya kuwania ushawishi miongoni mwa mataifa makubwa, ambayo yameongeza juhudi zao maradufu tangu mgogoro wa Ukraine uanze miezi 15 iliyopita

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha