Rais Xi Jinping asisitiza juhudi za kuharakishwa za kujenga nchi ya China kuwa inayoongoza katika elimu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2023

BEIJING – Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesisitiza kufanya juhudi za kuharakisha kuijenga China kuwa nchi inayoongoza katika elimu huku uongozi wa Chama ukiitisha semina elekezi siku ya Jumatatu.

Akiongoza semina elekezi ya wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Xi ambaye pia ni Rais wa China amesema lengo hilo ni utangulizi wa kimkakati wa kujenga nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote, ni mhimili muhimu wa kufikia kujitegemea zaidi na yenye nguvu zaidi katika sayansi na teknolojia, na ni njia bora ya kukuza ustawi wa pamoja kwa wote.

Rais Xi ametoa wito wa kuharakisha uboreshaji wa sekta ya elimu ili kutoa uungaji mkono mkubwa kwa ajili ya kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote.

China imejenga mfumo wa elimu mkubwa zaidi duniani na kujiunga na nchi zenye uchumi wa mapato ya juu ya kati katika suala la kiwango cha kufanya mambo ya kisasa katika elimu, Rais Xi amesema, huku akieleza kuwa China inashika nafasi ya 23 katika kiashiria cha ubora wa elimu duniani, ikipanda kwa nafasi 26 kutoka Mwaka 2012.

“Hii inadhihirisha kikamilifu kwamba njia ya elimu ya ujamaa wenye umaalum wa China ni sahihi kabisa,” amesema.

Amesema kuwa, ili kujenga nguvu ya China katika elimu, ni muhimu kutilia maanani uongozi wa jumla wa Chama juu ya elimu na kuchukulia kuitumikia kazi ya ustawishaji mkubwa wa Taifa la China kamajukumu kubwa .

Ameeleza kuwa madhumuni ya kujenga nchi ya China inayoongoza katika elimu ni kukuza vizazi vinavyofuatana vya watu wenye vipaji na uwezo wa kubeba wajibu na majukumu muhimu katika mchakato wa ujamaa wenye maendeleo ya kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha