Jeshi la Sudan na vikosi pinzani vyakubali kurefusha muda wa kusitisha mapigano kwa siku 5

(CRI Online) Mei 30, 2023

Jeshi la Sudan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF vimekubaliana kurefusha kwa siku tano muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano waliyosaini Mei 20 baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Pande hizo mbili zimesisitiza dhamira ya kuruhusu raia wote kuondoka kwa usalama kwenye maeneo yenye mgogoro na kulinda vifaa vya kiraia.

Hata hivyo mapigano makali yalizuka mjini Khartoum kati ya pande hizo mbili saa chache kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande hizo kufikia muda wake wa mwisho. Kwa mujibu wa mashuhuda, mapigano hayo yalitokea katika maeneo ya kaskazini mwa Khartoum, ambapo jeshi la Sudan lilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya RSF, huku RSF ikijibu kwa makombora ya kutungulia ndege.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha