Kahawa yaingia katika maeneo ya vijijini ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2023

Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa matumizi na manunuzi ya watu wa China katika utalii, mikahawa zaidi na zaidi iliyoanzia katika maeneo ya mijini imeanza kuonekana vijijini.

Takwimu kutoka mitandao ya kijamii ya China Meituan, Xiaohongshu na Douyin inathibitisha uhakika huu kikamilifu. "Ripoti ya Maendeleo ya Kipengele cha Kahawa Inayotengeneza papo hapo ya China ya Mwaka 2022" iliyotolewa na Meituan Gourmet inaonyesha kuwa oda za kahawa katika miji ya daraja la tatu zimeongezeka karibu mara mbili mwaka hadi mwaka, na oda za kahawa katika miji ya daraja la nne na la tano zimeongezeka kwa zaidi ya 250% mwaka hadi mwaka. Kumekuwa na zaidi ya post 30,000 kuhusu "Kahawa Kijijini" kwenye Mtandao wa Xiaohongshu, na mada #KahawaKijijini imefuatiliwa au kuchangiwa maoni zaidi ya mara milioni 8.96 kwenye Mtandao wa Douyin, ambao kimataifa unajulikana kama Tik Tok.

Katika Wilaya ya Anji, Mkoa wa Zhejiang, "idadi ya mikahawa kwa kila mtu" inazidi hata ile ya Shanghai. Mkahawa wa "Deep Blue Project" katika Kijiji cha Hongmiao, Wilaya ya Anji uko katika shimo la mgodi lililotelekezwa, sehemu ambayo ina ziwa la maji ya buluu na mawe. Watumiaji wa intaneti huita mahali hapa "Iceland Ndogo".

Mandhari nje ya mkahawa "Deep Blue Project"

Mandhari nje ya mkahawa "Deep Blue Project"

Katika siku ya tatu ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China Mwaka 2023, mkahawa wa "Deep Blue Project" uliuza vikombe 3,000 vya kahawa kwa siku moja, ukishika nafasi ya kwanza nchini China kwa idadi ya vikombe vya kahawa vilivyouzwa. Lakini, mkahawa uliopo katika eneo la Sanlitun, katikati ya Mji wa Beijing huuza vikombe 500 tu kwa siku.

Faida ya kupiga picha nzuri huwafanya vijana katika maeneo jirani ya Anji na hata mbali zaidi kuwa tayari kwenda kwenye mkahawa huo na kununua tikiti (pamoja na kikombe cha kahawa) kwa Yuan 68 (sawa na dola 10 hivi za Kimarekani).

Kahawa ya kijijini hutoa hisia nyingi zaidi, ambayo ni thamani ya kipekee inayotofautisha mikahawa ya vijijini na ile ya mijini.

Katika mchakato wa "kahawa +" kukutana na utamaduni wa vijijini, imeongeza "kahawa na mzazi-mtoto", "kahawa na hosteli", "kahawa na kupiga picha" na matukio mengine ya matumizi mchanganyiko katika maunuzi. Wakati huo huo, kahawa ya vijijini imekuwa daraja la kuunganisha vijana na vijiji kimwili na kiroho, na kusaidia vijiji kuendelea kustawishwa kupitia upendezeshaji wa mazingira, uboreshaji wa vifaa, na ongezeko la mapato.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha