Hali ya ikolojia ya China yaendelea kuwa bora Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2023

Picha hii iliyopigwa Machi 14, 2023 ikionyesha mandhari ya Ziwa Cuihu katika Eneo la Pujiang huko Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Xinhua/Xu Yu)

Picha hii iliyopigwa Machi 14, 2023 ikionyesha mandhari ya Ziwa Cuihu katika Eneo la Pujiang huko Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Xinhua/Xu Yu)

BEIJING - Ubora wa kiikolojia na mazingira wa China umedumisha mwelekeo wa kuwa bora Mwaka 2022, huku malengo ya kila mwaka yakifikiwa kwa mafanikio, Ofisa wa Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya China Jiang Huohua amesema Jumatatu.

Mwaka jana, hali ya hewa ya China ilikuwa tulivu na ubora wa maji ya juu ya ardhi uliendelea kuimarika, Jiang ameuambia mkutano na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wizara hiyo, ubora wa maji ya bahari chini ya mipaka ya China, hali ya mazingira ya udongo, mazingira ya kelele za mijini na hali ya kiikolojia kwa ujumla ilikuwa tulivu katika Mwaka 2022.

Katika kipindi hicho, ubora wa maji ya bahari uliongezeka kwa ujumla, huku uwiano wa maeneo yenye hali nzuri ya kufikia asilimia 81.9, ikiwa ni ongezeko la hadi asilimia 0.6 kutoka kwenye kiwango cha mwaka jana.

Akielezea kazi ngumu ya ulinzi wa ikolojia na mazingira nchini China, Jiang amesema juhudi zaidi zinapaswa kufanywa ili kuimarisha vita dhidi ya uchafuzi wa mazingira na kuimarisha kasi ya kuboresha ubora wa mazingira. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha