China kuendelea kuchangia kutafuta suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Ukraine

(CRI Online) Mei 30, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ming amesema pande zote zinazohusika na mgogoro wa Ukraine zimekubali mchango chanya wa China katika kuendeleza mazungumzo ya amani kuhusu mgogoro wa Ukraine, na kuongeza kuwa China itaendelea kutoa mchango wake katika utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

Bi. Mao amesema hayo wakati wa mkutano na wanahabari akieleza ziara za mjumbe maalum wa China katika masuala ya Ulaya na Asia Bw. Li Hui aliyetembelea Ukraine na nchi nyingine.

Kwenye ziara zake nchini Ukraine, Poland, Ufaransa, Ujerumani, makao makuu ya Umoja wa Ulaya na Russia kuanzia Mei 15 hadi 26, Bw. Li alishiriki katika mawasiliano ya kina na kubadilishana maoni na pande zote kuhusu utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Ukraine.

Msemaji huyo amesema mgogoro wa Ukraine bado uko katika wakati mbaya na China itaendelea kuimarisha mazungumzo ili kujenga maelewano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha