China na Afrika zahitaji zaidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano kuliko wakati wowote uliopita

(CRI Online) Mei 30, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema kwa sasa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani na likiwa bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, China na Afrika zinahitaji zaidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano kuliko wakati wowote uliopita.

Bi. Mao Ning amesema uhusiano kati ya China na nchi za Afrika umefika kwenye kiwango kipya, na kuingia kwenye kipindi kipya cha kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.

Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika, kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kushikilia kulinda maslahi halali ya kila upande, kuhimiza mambo ya kisasa yenye umaalumu wa kila upande, kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia, kujitahidi kutimiza usalama wa pamoja, kuimarisha mawasiliano na mabadilishano ya ustaarabu, ili moyo wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika uenziwe na kuenea nchini China na barani Afrika, kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja yenye kiwango cha juu na ya karibu zaidi, na kuweka mfano wa kuigwa kwa kuhimiza jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha