Xi Jinping atoa wito wa kuharakisha juhudi za kuhimiza mfumo na uwezo wa Usalama wa Taifa la China kuwa wa kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne alitoa wito wa kuharakisha juhudi za kuhimiza mfumo na uwezo wa usalama wa nchi kuwa wa kisasa.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, ya China (CMC) ameyasema hayo alipokuwa akiongoza mkutano wa kwanza wa Kamati ya Usalama wa Nchi chini ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC. Rais Xi ni mkuu wa kamati hiyo.

Ametoa wito wa kuendelea kufahamu kwa kina hali ngumu na changamoto zinazokabili usalama wa nchi na kufahamu kwa usahihi masuala muhimu ya usalama wa nchi .

Amehimiza juhudi za kulinda muundo mpya wa maendeleo wa China kwa usanifu mpya wa usalama na kupata maendeleo mapya ya kazi ya usalama wa nchi.

Mkutano huo ukifanya majumuisho kuhusu kazi ya kamati hiyo, umesema kamati hiyo imelinda kithabiti mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo, na usalama wa nchi umeimarishwa kwa pande zote.

Masuala ya usalama wa nchi ambayo China inakabiliana nayo leo "yanazingatiwa kuwa yenye utata zaidi na vigumu zaidi kutatuliwa," mkutano huo umesema. Umesisitiza ulazima wa kujiandaa ili kuwa tayari kukabiliana na hali mbaya na hali inayozidi kuwa mbaya kabisa na kuwa tayari kustahimili "pepo kali, maji ya mawimbi, na hata dhoruba hatari."

Mkutano huo umetoa wito wa kuchukua hatua ya kujenga mazingira mazuri ya usalama wa nje kwa China ili kulinda vyema kufungua mlango na kusukuma mbele mafungamano ya pande zote ya maendeleo na usalama.

Mkutano huo pia umetoa wito wa kufanyia marekebisho mbinu zinazotumika katika kulinda na kujenga muundo wa usalama wa nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha