Kuanza safari ya kibiashara ya Ndege ya C919 kunaleta fursa mpya kwa tasnia ya usafari wa anga ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023

Picha hii iliyopigwa Mei 28, 2023 ikionyesha ndege kubwa ya abiria ya C919 ambayo ni ya kwanza kuundwa na China yenyewe, ikijiandaa kwa safari yake ya kwanza ya kibiashara huko Shanghai, Mashariki mwa China. Ndege hiyo ya C919 ilianza safari yake ya kwanza ya kibiashara kutoka Shanghai hadi Beijing siku ya Jumapili, kuashiria kuingia kwake rasmi katika soko la usafiri wa anga. (Xinhua/Ding Ting)

Picha hii iliyopigwa Mei 28, 2023 ikionyesha ndege kubwa ya abiria ya C919 ambayo ni ya kwanza kuundwa na China yenyewe, ikijiandaa kwa safari yake ya kwanza ya kibiashara huko Shanghai, Mashariki mwa China. Ndege hiyo ya C919 ilianza safari yake ya kwanza ya kibiashara kutoka Shanghai hadi Beijing siku ya Jumapili, kuashiria kuingia kwake rasmi katika soko la usafiri wa anga. (Xinhua/Ding Ting)

BEIJING - Wakati ndege kubwa ya abiria ya C919 ambayo ni ya kwanza kuundwa na China yenyewe, imeingia katika huduma ya kibiashara, na tasnia ya usafiri wa anga nchini humo na sekta nyingine zinazoiunga mkono zitapata fursa kubwa za soko katika miongo ijayo, wachambuzi na wataalam wa sekta hiyo wamesema.

Ndege hiyo ya C919, yenye njia moja ya kutenganisha viti katika pande mbili ambayo imeundwa na Shirika la Ndege ya kibiashara la China (COMAC), ilikamilisha safari yake ya kwanza ya kibiashara kutoka Shanghai hadi Beijing siku ya Jumapili, kuashiria kuingia kwake rasmi katika soko la usafiri wa anga.

"Mafanikio kwa safari ya kwanza ya kibiashara ya Ndege ya C919 yanamaanisha kuwa ndege hiyo ya China imeingia kwenye soko kuu la ndege zenye viti 150 hadi 200 na njia moja ya kupita abiria, ambalo ni moja ya masoko yenye ushindani mkubwa katika sekta ya usafiri wa anga," mtaalamu wa masuala ya anga Han Tao ameliambia jarida la Security Daily.

Ukiwa ulizinduliwa Mwaka 2007, mradi wa C919 umeshuhudia ndege yake ya kwanza ikitoka kwenye kiwanda cha kuunda ndege Mwaka 2015. Mwaka 2017, modeli hiyo ya ndege ilifanya safari yake ya kwanza kwa mafanikio.

Ndege ya C919 imewekwa katika huduma ya kawaida na Shirika la Safari za Ndege la China Eastern siku ya Jumatatu, ikiruka kati ya Shanghai na Chengdu, Mkoa wa Sichuan. Shirika hilo limesema kwamba ndege mpya nyingi zaidi zikikabidhiwa, modeli hiyo ya ndege itafanya kazi kwenye njia nyingi zaidi za usafari wa anga kwa taratibu.

Hadi sasa kumekuwa na oda 1,061 za ndege za C919 kutoka kwa wateja mbalimbali, kwa mujibu wa COMAC.

Modeli ya C919 ina faida katika ufanisi na bei, limesema shirika la Cinda Securities, ambalo linatarajia usafiri wa kibiashara wa ndege hiyo kuongeza ushawishi wake sokoni.

Kwa mujibu wa makadirio ya soko yaliyotolewa na COMAC mwishoni mwa Mwaka 2022, China inatarajiwa kuwa soko kubwa zaidi la usafiri wa anga kwa nchi moja moja duniani ifikapo Mwaka 2041.

Katika kipindi cha 2022-2041, soko la usafiri wa anga la China litapokea ndege mpya 9,284, zikichukua asilimia 21.9 ya usafirishaji wote wa kimataifa, kwa mujibu wa COMAC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha