Tamthiliya na filamu za China zawa maarufu barani Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi inayoongezeka ya tamthiliya na filamu za China zimepata umaarufu mkubwa miongoni mwa watazamaji wa Afrika, zikitumika kama dirisha ambalo wanaweza kuielewa China vyema zaidi.

Hafla ya “Usiku wa Sauti na Video za China, Africa na Nchi za Kiarabu”, ikiwa ni sehemu ya msimu wa utangazaji wa tamthiliya za TV na filamu wa Beijing ambao uliandaliwa na Ofisi ya Redio na Televisheni ya Manispaa ya Beijing, ilifanyika kwenye mji huo hivi karibuni. Wakati wa hafla hiyo, sehemu za tamthiliya na filamu mbalimbali za China zilirekodiwa sauti za wasanii wahusika kwa Lugha za Kiingereza, Kireno, Kiswahili na lugha nyinginezo na wasanii kutoka Afrika na Asia Magharibi.

Wasanii wa kigeni wakirekodi sauti za wahusika wa sehemu ya tamthiliya ya Kichina ya kuoneshwa kwenye televisheni katika lugha yao ya kienyeji kwenye hafla ya Maudhui ya Video wa China, Africa na Nchi za Kiarabu, shughuli ya msimu wa utangazaji wa tamthiliya na filamu ya Beijing TV iliyofanyika Beijing, China. (Picha kwa hisani ya Kampuni StarTimes)

Wasanii wakirekodi sauti za wahusika wa sehemu ya tamthiliya ya Kichina ya kuoneshwa kwenye televisheni katika lugha yao ya kienyeji kwenye hafla ya Maudhui ya Video wa China, Africa na Nchi za Kiarabu, shughuli ya msimu wa utangazaji wa tamthiliya na filamu ya Beijing TV iliyofanyika Beijing, China. (Picha kwa hisani ya Kampuni StarTimes)

Shughuli ya msimu wa utangazaji wa tamthiliya za TV na filamu wa Beijing imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu 2014. Kupitia programu hii, zaidi ya vipindi bora 100 vya televisheni na filamu za China vimetangazwa katika zaidi ya nchi na maeneo 30, ikiwemo Uingereza, Brazili, Argentina, Russia, na Tanzania.

Katika kipindi hicho cha mwaka huu, watazamaji wa Afrika wanaweza kufurahia tamthiliya za China za TV kama vile "Hadithi ya Geti la Zheng Yang ", "Songa Mbele," na "Mume Wangu Shujaa," pamoja na tamthiliya za kuonyesha hali halisi na katuni.

Guo Ziqi ni naibu mkuu wa kampuni ys StarTimes ya China. Anasema tamthiliya za China zinazooneshwa kwenye televisheni barani Afrika zinapanuka, zikihusisha siyo tu tamthiliya na vipindi vya vijana vilivyowekwa katika nyakati za kisasa, lakini pia tamthiliya zinazohusu mambo ya kijeshi na kijasusi, maonyesho ya karate na tamthilia za fantasia.

"Wanafamilia wangu wote wanapenda tamthiliya za China kama vile 'Doudou na Mama Wakwe zake', 'Kuwa Mwanaume Bora', na 'Mwalimu Wangu wa Elimu ya Michezo'. Sehemu kubwa ya visa vya tamthilia hizi vinatuvutia kwa sababu vinahusiana na maisha ya kila siku ya watu wa kawaida," anasema Paula, mtazamaji kijana kutoka Gabon.

Katika kipindi cha miaka tisa iliyopita, aina mbalimbali za shughuli zenye mada mbalimbali kama vile maonyesho, vikao na mikutano ya mashabiki zimefanyika wakati wa msimu wa utangazaji wa filamu na tamthilia za TV wa Beijing katika nchi za Afrika. Shughuli hizi zimekuza uhusiano wa karibu kati ya watu wa China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha