FAO yasema asilimia 10 ya watu Duniani wanalala na njaa

(CRI Online) Mei 31, 2023

Takribani watu milioni 828 sawa na asilimia 10 ya idadi ya watu wote duniani wanalala njaa kila usiku, ikiwa ni asilimia 46 zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Takwimu hizo zimetolewa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kupitia ripoti yake ya hivi karibuni ambayo imesema, kati ya walioathiriwa na njaa, theluthi mbili ni wanawake na asilimia 80 wanaishi katika maeneo yanayoathiriwa vibaya na mabadiliko ya tabianchi.

Majanga na matatizo mbalimbali katika muongo uliopita yamesababisha kuongezeka kwa watu wenye njaa duniani katika miaka ya hivi karibuni. Kati ya mwaka 2019 na 2021, idadi ya watu wasio na lishe bora iliongezeka kwa zaidi ya milioni 150, sababu kuu ikiwa ni migogoro mbalimbali, mabadiliko ya tabianchi, majanga ya kiuchumi na janga la COVID-19.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha