Kuimarika kwa uchumi wa China, maendeleo ya kiteknolojia yatawanufaisha Waafrika wengi zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2023
Kuimarika kwa uchumi wa China, maendeleo ya kiteknolojia yatawanufaisha Waafrika wengi zaidi
Kwaku Amponsah Asiama, Mtendaji na Msaidizi wa Kisiasa wa Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha Ghana, New Patriotic Party, akizungumza katika mahojiano mjini Accra, Ghana, Mei 10, 2023. Kuimarika kwa kasi kwa uchumi na maendeleo ya kiteknolojia ya China kutaleta manufaa zaidi kwa watu wa Afrika, mwanasiasa wa Ghana amesema. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Kuimarika kwa kasi kwa uchumi na maendeleo ya kiteknolojia ya China kutaleta manufaa zaidi kwa watu wa Afrika, Kwaku Amponsah Asiama, Mtendaji na Msaidizi wa Kisiasa wa Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha Ghana, New Patriotic Party amesema.

Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni, Asiama amesema mtazamo wake huo unachagizwa na uchunguzi wake wa karibu nchini China, maisha na uzoefu wa kazi barani Afrika, na imani katika ushirikiano unaoendelea kati ya pande hizo mbili.

Mwezi Aprili, Asiama alishiriki katika Tamasha la 7 la vijana kati ya China na Afrika lililofanyika nchini China akiwa mwakilishi pekee wa vijana wa Ghana, ambapo alitembelea miji na miradi mbalimbali ya China kwa mara ya kwanza na kutoa mawazo yake kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika na wawakilishi wengine.

"Ilikuwa moja ya uzoefu bora zaidi ambao nimepata katika maisha yangu kama mtu binafsi. Nimevutiwa sana na kila kitu nilichokiona nchini China, na jinsi mambo yamefanyika nchini China," amesema, huku akiipongeza nchi hiyo kwa ukarimu, mazingira mazuri, na uchumi wake imara.

Asiama amesema anashangazwa na fahari ya Ukuta Mkuu wa China na Mlima Taishan, na mandhari ya watalii ndani na nje ya China sasa wakimiminika kwenye vivutio hivyo vinavyojulikana vya utalii, na kuakisi kushamiri kwa sekta ya utalii ya China.

Kwa mujibu wake, kuimarika kwa sekta ya utalii ni ishara nzuri kwa uchumi wa China kwani kunaweza kuchochea ukuaji katika sekta nyingine nyingi kama vile chakula, ukarimu na usafirishaji.

"Lazima niipongeze China kwa hili; ni wazi bado ni miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani. Mambo yamerejea katika hali ya kawaida, na yanakwenda kwa kasi kubwa sana kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa katika kiwango cha kawaida." Asiama amesema.

Akielezea treni ya mwendo kasi ya China kuwa ya kiwango cha juu, Asiama amesema anashangazwa na jinsi watu wa China walivyotumia hekima na ubunifu wao kutatua matatizo ya usafiri ya wakazi katika mchakato wa ukuaji wa miji, ambao pia unatoa uzoefu muhimu kwa Afrika, bara lenye idadi kubwa ya watu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali katika usafiri.

"Ukiangalia ubora wa barabara zinazojengwa (na Wachina) katika nchi nyingi za Afrika, hakuna tofauti na kile tunachokiona China," amesema na kusisitiza kwamba safari yake hii iliimarisha wazo lake kwamba miradi inayojengwa na Wachina kila wakati kutoa moja ya miradi bora chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha