Serikali ya Tanzania yapanga kuongeza kodi ya mafuta ya kula yanayoingizwa nchini humo

(CRI Online) Mei 31, 2023

Wizara ya Kilimo nchini Tanzania inafanya mazungumzo na Wizara ya Fedha na Mipango kuangalia njia za kuongeza kodi kwa mafuta yanayoagizwa kutoka nje ya nchi ili kukabiliana na kuporomoka kwa bei ya mafuta nchini humo.

Hayo yamesemwa jana Jumatatu bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde, ambaye amesema Wizara yake na Wizara ya Fedha na Mipango zinaangalia namna bora ya kutatua changamoto hiyo, ikiwemo kuangalia sera za fedha, na hasa katika kuboresha wigo wa kuongeza kodi kwa mafuta ambayo yanaagizwa kutoka nje ya nchi ili kuwalinda wakulima nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha