Tanzania kukomesha kukatika kwa umeme mara kwa mara ifikapo 2025/2026

(CRI Online) Juni 01, 2023

Waziri wa Nishati wa Tanzania Bw. January Makamba amesema Tanzania itakomesha kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo mengi ya nchi hiyo katika muda wa miaka miwili hadi mitatu ijayo, baada ya kukamilika kwa mitambo kadhaa ya kuzalisha umeme inayoendelea kujengwa.

Akiongea bungeni mjini Dodoma Bw. Makamba amesema Kituo cha Bwawa la Kuzalisha umeme kwa maji la Julius Nyerere chenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115 kinaendelea kujengwa, na ujenzi wake ukiwa umefikia asilimia 87.

Pia amesema mtambo wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua unatarajiwa kuanza kujengwa mkoani Shinyanga, na pia mipango iko katika hatua za mwisho za kutekeleza miradi ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo katika mikoa ya Singida na Kilimanjaro, na miradi yote iliyopangwa ya kuzalisha umeme itaunganishwa kwenye gridi ya Taifa.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha