Mradi wa kwanza wa China wa baharini wenye uwezo wa kuhifadhi kaboni ya uzito wa tani milioni waanza kufanya kazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2023

Picha hii ikionyesha vifaa katika jukwaa la mafuta la Enping 15-1 lililoko umbali wa kilomita 200 Kusini-Magharibi mwa Shenzhen, China, Mei 31, 2023. (Xinhua/Mao Siqian)

Picha hii ikionyesha vifaa katika jukwaa la mafuta la Enping 15-1 lililoko umbali wa kilomita 200 Kusini-Magharibi mwa Shenzhen, China, Mei 31, 2023. (Xinhua/Mao Siqian)

BEIJING - Mradi wa kwanza wa China wa baharini wenye uwezo wa kuhifadhi hewa ya kaboni yenye uzito wa tani milioni umeanza kufanya kazi Alhamisi katika Bahari ya China ya Kusini, kwa mujibu wa Shirika la Taifa la Mafuta Baharini la China (CNOOC).

Mradi huo umeundwa kuhifadhi hewa ya carbon dioxide (CO2) yenye uzito wa jumla wa zaidi ya tani milioni 1.5, ambayo ni sawa na kupanda karibu miti milioni 14, shirika hilo limesema.

Mradi huo, unaohudumia jukwaa la mafuta la Enping 15-1 lililoko umbali wa kilomita 200 Kusini-Magharibi mwa Mji wa Shenzhen, unakamata na kuchakata hewa ya carbon dioxide kutoka maeneo ya mafuta na kisha kuingiza hewa hiyo kwenye muundo wa kijiolojia wa "kuba" kwa kina cha karibu mita 800 chini ya bahari na karibu kilomita 3 kutoka kwenye jukwaa.

Kuanza kufanya kwa mradi huo kunaashiria mafanikio ya China katika kupata seti kamili ya teknolojia na vifaa vya kunasa, kusindika, kuingiza, kuhifadhi na kufuatilia hewa ya carbon dioxide baharini.

Pia inafungua safari mpya kwa China kutimiza lengo lake la "kaboni pacha" la kufikia kilele cha utoaji wa hewa ya kaboni ifikapo Mwaka 2030 na kufikia usawazishaji katika kutoa hewa ya kaboni ifikapo Mwaka 2060, shirika hilo limesema.

Kwa msingi wa mradi huu, CNOOC imeanzisha mradi wa kwanza wa China wa kukamata na kuhifadhi kaboni yenye uzito wa tani milioni 10 huko Huizhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, na itakamata carbon dioxide inayotolewa katika Ghuba ya Daya na kuisafirisha hadi eneo la bahari la Mdomo wa Bonde la Mto Pearl kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Teknolojia imekuwa nguvu ya kutimiza lengo la China katika kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni.

Picha  hii iliyopigwa kutoka angani ikionyesha jukwaa la mafuta la Enping 15-1 lililoko umbali wa kilomita 200 Kusini Magharibi mwa Mji wa Shenzhen,China, Mei 31, 2023. (Xinhua/Mao Siqian)

Picha hii iliyopigwa kutoka angani ikionyesha jukwaa la mafuta la Enping 15-1 lililoko umbali wa kilomita 200 Kusini Magharibi mwa Mji wa Shenzhen,China, Mei 31, 2023. (Xinhua/Mao Siqian)

Picha hii iliyopigwa kutoka angani ikionyesha jukwaa la mafuta la Enping 15-1 lililoko umbali wa kilomita 200 Kusini Magharibi mwa Mji wa Shenzhen,China, Juni 1, 2023. (Xinhua/Mao Siqian)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha