Rais wa Kenya azindua huduma ya mikopo ya kidijitali kwa vikundi wakati taifa likiadhimisha miaka 60 ya uhuru

(CRI Online) Juni 02, 2023

Kenya Alhamisi ilizindua huduma ya mikopo ya kidijitali kwa vikundi na Asasi za Kijamii za Kuweka na Kukopa (Saccos) wakati nchi hiyo ikiadhimisha miaka 60 ya uhuru, Siku ya Madaraka.

Rais William Ruto, ambaye alizindua huduma hiyo ya kidijitali, amesema bidhaa hiyo iliyopewa jina la Mikopo ya Vikundi vya Wachuuzi, itawapa wanachama uhuru wa kiuchumi kama ilivyotarajiwa na waanzilishi wa Kenya.

Akiongea siku hiyo ya Madaraka, Ruto alisema chini ya Mikopo ya Vikundi vya Wachuuzi, watakuwa wakivipa vikundi fedha kati ya shilingi 20,000 (dola 144 za U.S.) na shilingi milioni 1. Amebainisha kuwa wanataka kuhakikisha kuwa vikundi hivi vinajihusisha na biashara na kutoa nafasi za ajira.

Rais Ruto amesema zaidi ya Wakenya milioni 20 walijiandikisha kwenye mikopo ya awali, ambapo zilitolewa takriban dola milioni 216, huku dola milioni 142 zikiwa zimesharejeshwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha