Baraza la Usalama launga mkono uwepo wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan

(CRI Online) Juni 02, 2023

Baraza la Usalama limeeleza kuunga mkono kuendelea kuwepo kwa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan (UNITAMS) ili kusaidia hali ya nchini humo na katika nchi jirani, na linatazamiwa kuongeza tena muda wa mamlaka ya tume hiyo ambao unamalizika siku ya Jumamosi.

Akiongea na wanahabari Lana Zaki Nusseibeh, mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Umoja wa Mataifa, na ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama kwa mwezi Juni, amesema katika mashauriano ya faragha yaliyofanyika Jumatano kuhusu hali ya Sudan kwamba, kulikuwa na uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa wajumbe wa baraza juu ya kazi ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan.

Amesema suala hilo kwa sasa linajadiliwa, na kama Rais wa Baraza la Usalama, UAE iko tayari kupanga mkutano wa kupiga kura juu ya kuongezwa kwa muda wa UNITAMS.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha