

Lugha Nyingine
Nchi nyingi za Asia-Pasifiki hazikaribishi uwepo wa NATO barani Asia: Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China
BEIJING - Nchi nyingi za Asia-Pasifiki hazikaribishi uwepo wa Jumuiya ya NATO barani Asia na hakika hazitaruhusu Vita Baridi au vita moto kutokea tena barani Asia, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema Jumatatu.
Wang alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu kauli za viongozi wa nchi nyingi zikiwemo Indonesia na Singapore kwamba hawataki kuona "Vita baridi vipya" au kulazimishwa kuchagua upande mmoja kati ya China na Marekani wakati wa mkutano wa hivi majuzi wa Mazungumzo ya Shangri-La.
Wang amesema, kauli hizo ni dalili tosha kwamba nchi nyingi za eneo hili zimetahadharishwa na kupinga jaribio la nchi fulani kuanzisha "Vita Baridi vipya" katika Asia na kuzilazimisha nchi za eneo hilo kuchagua upande.
Kile nchi zinachotaka katika eneo hili ni kudumisha uhuru wa kimkakati na kudumisha utulivu na ustawi wa eneo hilo.
Amesema, kinachofuatiliwa zaidi ni kwamba baadhi ya nchi, huku zikidai kutetea uhuru na uwazi na zinalenga kulinda amani na ustawi katika eneo hilo, kwa kweli zimekuwa zikiunda kambi mbalimbali za kijeshi na kupanua ushawishi wa NATO katika eneo la Asia-Pasifiki.
Wang amesema, mtazamo wa nchi nyingi katika eneo hilo uko wazi sana. Zinapinga kuibuka kwa kambi za kijeshi katika kanda hiyo, hazikaribishi uwepo wa NATO katika Asia, hazitaki mfano wa mapambano ya kambi kutokea barani Asia, na kwa hakika hazitaruhusu Vita Baridi au vita moto kutokea tena Asia.
"Asia ni kanda yenye nguvu zaidi kiuchumi na yenye matumaini duniani, inaweza kutoa jukwaa kubwa la ushirikiano wa kunufaishana, na haipaswi kugawanywa kuwa kambi zilizotengwa za kipekee" msemaji huyo amesema, akibainisha kuwa nchi za Asia zinakaribisha jitihada za pamoja kufanikiwa pamoja na hazikaribishi mipango ambayo inaweza kuleta matatizo katika kanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma