Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu aonya kuhusu madhara ya uharibifu wa bwawa la Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2023

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu na Mratibu wa Misaada ya Dharura Martin Griffiths (Mbele) akizungumza katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Ukraine kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 6, 2023. (Eskinder Debebe/Picha ya UN / Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu na Mratibu wa Misaada ya Dharura Martin Griffiths ameonya siku ya Jumanne kuhusu madhara makubwa ya uharibifu wa bwawa la kuzalisha umeme kwa maji la Kakhovka, Kusini mwa Ukraine.

Griffiths ameuambia mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, uharibifu wa bwawa hilo huenda ni tukio kubwa zaidi la uharibifu wa miundombinu ya kiraia tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine Februari 2022.

"Ukubwa kamili wa tukio hilo utajitokeza na kujulikana kikamilifu katika siku zijazo. Lakini tayari ni wazi kuwa litakuwa na madhara makubwa na yasiyoweza kuhimilika kwa maelfu ya watu Kusini mwa Ukraine," amesema.

Amesema, bwawa la Kakhovka, ni njia ya kuokoa maisha katika eneo hilo na chanzo muhimu cha maji kwa mamilioni ya watu, siyo tu katika Kherson lakini pia katika mikoa ya Zaporizhzhia na Dnipro.

Bwawa hilo ni chanzo kikuu cha kilimo cha umwagiliaji Kusini mwa Kherson na peninsula ya Crimea. Mafuriko yanayoendelea yataathiri shughuli za kilimo, kuharibu mifugo na uvuvi, na kuleta madhara ya muda mrefu. Hili ni pigo kubwa kwa sekta ya uzalishaji wa chakula ambayo tayari imeharibiwa kwa kiasi kikubwa, amesema Griffiths.

Serikali ya Ukraine imeripoti kwamba takriban makazi 40 tayari yamejaa mafuriko au kwa sehemu kuleta mafuriko katika eneo la Kherson. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo. Athari kubwa pia itatokea katika maeneo yanayodhibitiwa na Russia, ambapo wasaidizi wa kibinadamu bado wanajitahidi kupata ufikiaji, amesema Griffiths huku akitaja uwezekano mkubwa wa madhara katika uzalishaji umeme na kwenye mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhia.

“Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu tayari yameongeza oparesheni kujaribu kushughulikia athari za tukio hilo. Mwitikio wa dharura unaendelea ili kutoa msaada wa haraka kwa zaidi ya watu 16,000 walioathirika,” amesema.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano wa dharura kuhusu hali ya Ukraine kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 6, 2023. (Eskinder Debebe/Picha ya UN/ Xinhua)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano wa dharura kuhusu hali ya Ukraine kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 6, 2023. (Eskinder Debebe/Picha ya UN/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha