

Lugha Nyingine
Jumuiya ya kimataifa yahimiza ushirikiano katika usimamizi wa taka barani Afrika
Maafisa wa serikali, viongozi wa kisekta na watafiti wamekutana Jumanne pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Makazi unaoendelea jijini Nairobi, Kenya, ili kutafuta uungaji mkono wa kuhimiza uchakataji wa taka pamoja na kutoa nafasi za ajira katika kukuza uchumi wa mzunguko.
Washiriki hao wamejadiliana kuhusu ushirikiano katika kukuza usimamizi bora wa taka kwa nchi za Afrika ili kuhifadhi mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu wa Kenya, Festus Ng'eno, amesema sera thabiti pamoja na ufadhili, matumizi ya teknolojia na ubunifu, ni mambo muhimu katika kukuza uchumi wa mzunguko wa Afrika.
Naye afisa mtendaji mkuu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, John Bosco Kalisa, amesema kuwa usimamizi endelevu wa taka ni muhimu katika kufikia mustakabali wa kijani, uhimilivu, ustawi na ujumuishaji kwa miji ya Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma