Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi:  Pambo la kumbukumbu ya kiwanda cha chuma cha pua chenye historia ya miaka mia moja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2023

Mwezi Juni, 2016, wafanyakazi wa Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo cha Serbia walimzawadia Rais Xi Jinping wa China pambo la  kumbukumbu  yenye picha ya kiwanda hicho. (Picha na Hu Yang)

Mwezi Juni, 2016, wafanyakazi wa Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo cha Serbia walimzawadia Rais Xi Jinping wa China pambo la kumbukumbu yenye picha ya kiwanda hicho. (Picha na Hu Yang)

Mwezi Juni, 2016, wakati Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara nchini Serbia, alikwenda kutembelea Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo. Wafanyakazi walitumia chuma cha pua kilichozalishwa na kiwanda chao "kutengeneza mahsusi" zawadi moja kwa Rais Xi -- pambo la kumbukumbu yenye picha ya Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo. Zawadi hii iliyotengenezwa kwa chuma cha pua imeweka kumbukumbu kuhusu simulizi ya kiwanda hicho chenye historia ya miaka mia moja ambacho kimefufuka kwa msaada wa China.

Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo kilikuwa kiwanda kikubwa cha kiserikali nchini Serbia. Wakati wa ustawi wake, kilichangia 40% ya mapato ya fedha ya mji. Kazi na maisha ya wakazi walio karibu theluthi moja yalihusiana moja kwa moja na kiwanda hiki kikubwa. Hata hivyo, mwishoni mwa miaka ya 1990, kutokana na kushuka kwa uwezo wake wa ushindani, kiwanda hiki kilikumbwa na taabu kubwa. Ili kuokoa kiwanda hiki, serikali ya Serbia ilipanga na kutangaza raundi kadhaa za zabuni za kimataifa, lakini hakuna hata moja iliyofaulu. Vucic, ambaye alikuwa waziri mkuu wa Serbia wakati huo, alisema, "Mwishowe, washirika wetu wa China wametuletea matumaini ya kweli."

Mnamo Aprili 2016, kwa kutumia fursa ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", Kundi la Kampuni za Hegang la China (HBIS) liliwekeza euro milioni 46 kuchukua umiliki wa Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo na kuanzisha Kampuni tanzu ya Chuma cha Pua ya Serbia. Katika muda usiofikia nusu mwaka baada ya hapo, kiwanda hicho kilibadilisha hali ya kula hasara kuwa kupata faida. Mwaka 2018, kiwanda hicho kilikuwa muuzaji nje mkubwa zaidi wa bidhaa nchini Serbia, na chuma chake cha pua chenye ubora wa juu kinasafirishwa nchi na maeneo hadi zaidi ya 30, na zaidi ya wafanyakazi 5,000 waliokuwa wenye ukosefu wa ajira sasa wamerudi kwenye karakana.

Katika nchi zilizo kando ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuna mifano mingi inayofanana na hali ya kufufuka ya Kiwanda cha Chum cha Pua cha Smederevo. Sasa, mashirika ya serikali ya China yameshiriki katika ujenzi wa miradi zaidi ya 3,400 kando ya "Ukanda Mmoja, Njia moja".

Juni 19, 2016, Rais Xi Jinping wa China alitembelea Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo kilichomilikiwa na Kundi la Kampuni za Hegang (HBIS) huko Belgrade, nchini Serbia. Picha hii ikionyesha Rais Xi akitoa hotuba katika Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo. (Picha na Ding Lin)

Juni 19, 2016, Rais Xi Jinping wa China alitembelea Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo kilichomilikiwa na Kundi la Kampuni za Hegang (HBIS) huko Belgrade, nchini Serbia. Picha hii ikionyesha Rais Xi akitoa hotuba katika Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo. (Picha na Ding Lin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha