

Lugha Nyingine
China yapinga serikali ya Japan kutiririsha maji taka ya kituo cha kuzalisha umeme kwa nyuklia cha Fukushima baharini
(CRI Online) Juni 08, 2023
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema, ingawa serikali ya Japan inasisitiza kusema maji taka yaliyotoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima hayana sumu, na kumwaga maji hayo baharini ni chaguo pekee, lakini habari zilizotolewa na vyombo vya habari vya Japan, zinaeleza kuwa samaki wa baharini waliovuliwa kwenye bandari ya kituo hicho wamevuka viwango stahiki vya mionzi ya sumu.
Bw. Wang amesisitiza kuwa hatua hiyo ya ubinafsi ya Japan inaharibu maslahi ya pamoja ya binadamu, kuathiri vibaya raia wa nchi jirani na nchi za visiwa vya bahari ya Pasifiki, na kupunguza uaminifu wa Japan duniani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma