"kahawa ya kiubunifu" imekuwa  ongezeko jipya kwenye soko la kahawa la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2023

Kahawa ya Latte ya maparachichi na maziwa ya coconut, Kahawa ya Latte ya Tofu Pudding, Kahawa ya Americano inayotiwa The Dark Plum Sauce, Kahawa ya Americano inayotiwa Ginseng...Katika hali ya ushindani unaozidi kuwa mkali kwenye soko la kahawa nchini China, chapa nyingi za kahawa zinajaribu kuvutia watumiaji kwa kupitia vinywaji vya kahawa vyenye hali mpya ya kiubunifu, "Kila kitu + Kahawa" kinakuwa nenosiri la wafanyabiashara kwa kuvutia watumiaji.

Picha hii ikionyesha Kahawa Maalum yenye Ladha ya litchi na rose, ambayo rangi yake itakuwa ya waridi kutoka zambarau iliyofifia baada ya kuwekwa kwa muda. (Picha na Sina Fedha)

Picha hii ikionyesha Kahawa Maalum yenye Ladha ya litchi na rose, ambayo rangi yake itakuwa ya waridi kutoka zambarau iliyofifia baada ya kuwekwa kwa muda. (Picha na Sina Fedha)

Katika shughuli maalum ya Siku ya Utamaduni wa Kahawa ya Changning 2023 lililofanyika Shanghai muda mfupi uliopita, "Kahawa Maalum" ambazo zimeendelea kupata umaarufu katika miaka ya hivi karibuni zilivutia watu wengi, zikiwemo kahawa maalum inayoweza kubadilisha rangi yenye Ladha ya litchi na rose, na kahawa maalum yenye divai. Kabla ya hapo, mkahawa mmoja wa Shanghai pia ulionekana kwenye utafutaji moto wa Weibo mara mbili kutokana na kutolewa kwa kinywaji kipya cha "Kahawa ya Latte ya Soy Sauce" na "Wali unaowekwa kwenye Kahawa".

Wafanyabiashara wengine wa kahawa pia wamepata ufunuo kutoka kwa vyakula vya Kichina. Kwa mfano, huko Yuncheng, mkoani Shanxi, kahawa ikichanganywa na siki ya Shanxi ikawa Kahawa ya Americano ya Siki yenye ladha ya chachu ya kuvutia. Huko Nanjing, mkoani Jiangsu, nyama ya bata iliyohifadhiwa kwa chumvi pia ilikuwepo kwenye kinywaji cha kahawa.

Mbali na chapa za kahawa, soko linaloshamiri la kahawa pia limevutia wafanyabiashara kutoka nyanja nyingine kujiunga na ushindani wa biashara hii . "Zhima Afya" ambayo ni chapa ya dawa za kijadi za China ya Tongrentang imejulikana kwa sababu ya kutolewa kwa kahawa yenye dhana ya kutunza afya kwa kutumia dawa za kijadi za China kama vile Kahawa ya Latte ya Wolfberry na Kahawa ya Americano ya Momordica Grosvenori.

Picha hii ikionyesha benchi la kazi la kutengeneza kahawa za mitishamba katika "Duka la Kwanza la Zhima Afya". (Picha na tovuti la Gazeti la Umma)

Picha hii ikionyesha benchi la kazi la kutengeneza kahawa za mitishamba katika "Duka la Kwanza la Zhima Afya". (Picha na tovuti la Gazeti la Umma)

Mwelekeo wa kuandaa aina mpya mbalimbali za Kahawa zilizo kama Chai ya Maziwa na wa Cocktail umeendelea kuwa na hali motomoto katika soko la kahawa la China, na umesababisha mabishano kati ya watendaji na watumiaji. Baadhi ya watu wanakosoa kutolewa kwa kahawa ya kiubunifu ni ujanja wa biashara, lakini waendeshaji wengi wa maduka ya kahawa wana maoni ya wazi ya kupenda kufuata hali ilivyo ya sasa. Huko Shanghai, ambayo ni mji maarufu kwa utamaduni wake wa kahawa, mwendeshaji wa duka moja la kahawa alisema kuwa, "kahawa ya kiubunifu" inaonyesha umaarufu wa utamaduni wa kahawa huko Shanghai. " Kama maduka ya kahawa yatakuwa mengi ya kutosha, matumizi yake ni yenye urahisi zaidi, umati wa watumiaji watakuwa wengi zaidi, na bei zitakuwa nafuu zaidi, ndipo watu wengi wanaweza kupokea hali ilivyo ya sasa ya kuwepo kwa kahawa za aina mbalimbali tofauti."

Kahawa ya aina ya kiubunifu imeashiria pembe ndogo ya mchakato wa kujaribu kuviandaa vinywaji vya kahawa viwe vya kienyeji nchini China. Hivi leo, baada ya kahawa kuingia China kwa miaka zaidi ya mia moja, kahawa bado inaendelea kutafuta njia ya kujiendeleza na kuwawezesha wachina wengi zaidi ambao hawana desturi ya kunywa kahawa waikubali na kuipenda kahawa. Kwenye kikombe kidogo cha kahawa, utamaduni wa China na tamaduni za duniani zinagongana kila wakati, na China inajaribu kuandaa kahawa yenye ladha ya kipekee ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha