

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akutana na mwenzake wa Palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al-Maliki mjini Beijing, China, Juni 13, 2023. Al-Maliki ameambatana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas katika ziara yake ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Yin Bogu)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al-Maliki mjini Beijing siku ya Jumanne.
Al-Maliki ameambatana na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ambaye yuko katika ziara yake ya kiserikali nchini China kuanzia Juni 13 hadi 16.
Qin amesema kuwa, Rais Abbas ndiye kiongozi mkuu wa kwanza kutoka kanda inayozungumza Lugha ya Kiarabu kukaribishwa nchini China mwaka huu, hali ambayo imeonesha vya kutosha urafiki maalum kati ya pande hizo mbili na uungaji mkono wa China kwa lengo kuu la haki la Palestina.
Amesema anaamini viongozi wakuu wa pande hizo mbili watapanga maendeleo ya baadaye ya uhusiano wa pande mbili na kuendeleza urafiki wa jadi kwenye kiwango cha juu.
"China daima imekuwa ikiunga mkono kithabiti lengo kuu la jihadi ya watu wa Palestina ya kurejesha haki zao halali za kitaifa, na itaendelea kuunga mkono mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel na kuchangia hekima katika kutatua suala la Palestina," Qin amesema.
Kwa upande wake Al-Maliki amesema kuwa China ni rafiki mwaminifu, wa kutegemewa, na Palestina inathamini mapendekezo yaliyotolewa na kiongozi mkuu wa nchi ya China Xi Jinping kwa ajili ya kutatua suala la Palestina.
Ameongeza kuwa Palestina inafuata sera ya kuwepo kwa China moja na itaendelea kuiunga mkono China katika masuala yanayohusu maslahi makuu ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma