Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang afanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Antony Blinken

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 19, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing, China, Juni 18, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing, China, Juni 18, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing siku ya Jumapili.

Qin amedokeza kuwa uhusiano kati ya China na Marekani uko katika kiwango cha chini kabisa tangu kuanzishwa kwake na kwamba hali hii hailingani na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili au kukidhi matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

“Sera ya China kuhusu Marekani bado ni thabiti. Kimsingi inaongozwa na kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wa kunufaishana zilizotolewa na Rais Xi Jinping. Kanuni hizi zinapaswa pia kuzingatiwa kama moyo unaoshikiliwa pamoja, mstari mwekundu wa kulindwa na lengo la kufuatwa kwa pamoja na pande zote mbili” amesema.

Amesema, China imejitolea kujenga uhusiano thabiti, unaotabirika na wa kiujenzi na Marekani, ikitumai kuwa Marekani itakubali mtazamo sahihi na wenye busara wa China, kushirikiana na China katika mwelekeo huo huo, kudumisha msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani, na kushughulikia matukio yasiyotarajiwa kwa utulivu, kitaalamu na busara.

Amesema kuwa, pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza na kutoa matokeo juu ya makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na Rais Xi na Rais Biden huko Bali kwa vitendo na moyo, na kufanya kazi ili kuleta utulivu na kurudisha uhusiano kwenye njia sahihi.

Huku akihimiza upande wa Marekani kuzingatia kanuni ya kuwepo kwa China moja na nyaraka husika, Qin amefafanua msimamo thabiti wa China na kuibua matakwa ya wazi juu ya suala la Taiwan na maslahi mengine ya kimsingi na masuala makuu. Qin ameeleza kuwa suala la Taiwan ndilo kiini cha maslahi ya kimsingi ya China, suala muhimu zaidi na hatari inayojulikana zaidi katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Pande hizo mbili zilikuwa na mazungumzo ya wazi, ya kina na ya kiujenzi kwa kirefu kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala muhimu.

Pande zote mbili zimekubaliana kutekeleza kwa pamoja maelewano muhimu ya pamoja yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili huko Bali, kudhibiti ipasavyo tofauti, na kuendeleza mazungumzo, mabadilishano na ushirikiano.

Pande zote mbili zimekubali kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu. Waziri Blinken amemwalika mwenzake Qin kutembelea Marekani, na Qin ameonyesha utayari wake wa kufanya ziara hiyo kwa wakati unaofaa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing, China, Juni 18, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing, China, Juni 18, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha