

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China Li Qiang atoa wito wa maendeleo mapya katika uhusiano kati ya China na Ujerumani
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Brandenburg mjini Berlin, Ujerumani, Juni 18, 2023. Kwa mwaliko wa Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Waziri Mkuu Li amewasili Ujerumani kwa ajili ya mashauriano ya saba kati ya serikali ya China na Ujerumani na kufanya ziara rasmi. (Xinhua/Huang Jingwen)
BERLIN - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amewasili Berlin, Ujerumani siku ya Jumapili kwa ziara rasmi nchini Ujerumani, ambapo pia atafanya duru ya 7 ya mkutano wa mashauriano kati ya serikali ya China na Ujerumani.
Alipowasili, Waziri Mkuu Li alisema Beijing iko tayari kushirikiana na Berlin kutafuta zaidi uwezo wa ushirikiano na kusukuma maendeleo mapya katika uhusiano wa pande mbili.
Waziri Mkuu Li amebainisha kuwa Ujerumani ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu awe waziri mkuu wa China, na ziara hii itaendeleza urafiki wa jadi wa nchi hizo mbili, na kuimarisha ushirikiano wao.
Amesema, mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China alipongezana na kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ujerumani, na kutoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa pande hizo mbili.
Waziri Mkuu Li amesema katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Ujerumani umekuwa na maendeleo thabiti, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kuimarishwa na kupanuliwa, ambapo mafanikio mapya yamepatikana katika sekta za uchumi na biashara, teknolojia, mawasiliano kati ya watu na ya kitamaduni, pamoja na maendeleo ya kijani.
Amedokeza kuwa duru ya 7 ya mkutano wa mashauriano kati ya serikali ya China na Ujerumani ni ya mara ya kwanza kukutanisha serikali mpya zilizoundwa za nchi hizo mbili na kufanya mawasiliano kwa mtindo wa kuangazia pande zote.
Amesema, upande wa China uko tayari kufanya mazungumzo ya uwazi na ya kina na upande wa Ujerumani kwa kufuata kanuni za kuheshimiana, kutafuta maoni ya pamoja huku tofauti zikiwekwa pembeni, na kupata manufaa ya pande zote na matokeo ya kunufaishana, ili kutafuta zaidi uwezekano wa ushirikiano, kushughulikia tofauti ipasavyo, na kuimarisha ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote, ili kutoa ishara yenye nguvu ya kudumisha minyororo thabiti ya usambazaji bidhaa wa kimataifa na amani na ustawi wa Dunia.
Akiwa Ujerumani, Waziri Mkuu Li atakutana na Rais wa Ujerumani Steinmeier, mwenyekiti wa mashauriano ya saba kati ya serikali ya China na Ujerumani pamoja na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani, kuhudhuria mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi na Kiufundi kati ya China na Ujerumani na mkutano wa majadiliano wa wajasiriamali wa China na Ujerumani, kukutana na wajumbe kutoka jumuiya za waendeshaji viwanda na wafanyabiashara za Ujerumani, na kutembelea kampuni za Ujerumani katika Jimbo la Bavaria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma