Kenya na EU zakamilisha mazungumzo kuhusu mpango wa ushirikiano wa kiuchumi

(CRI Online) Juni 20, 2023

Kenya na Umoja wa Ulaya (EU) Jumatatu zilikamilisha mazungumzo ya kisiasa ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) ambayo yatakuza biashara ya bidhaa na kutoa fursa mpya za kiuchumi.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa Nairobi nchini Kenya, kati ya Makamu wa Rais wa Tume Tendaji ya Ulaya ambaye pia ni Kamishna wa Biashara Valdis Dombrovskis na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Moses Kuria, yatarahisisha biashara na uwekezaji kati ya EU na Kenya.

Kwenye taarifa yao ya pamoja viongozi hao wamesema ni mpango kabambe wa biashara kati ya EU na nchi inayoendelea linapokuja suala la maendeleo endelevu kama vile tabianchi na ulinzi wa mazingira na haki za wafanyakazi.

Kwa mujibu wa takwimu, EU ni soko kubwa zaidi la mauzo ya nje ya Kenya na mshirika mkubwa wa pili wa kibiashara, ambapo thamani ya biashara yake katika mwaka 2022 ni jumla ya dola za Kimarekani bilioni 3.6, likiwa ni ongezeko la asilimia 27 ikilinganishwa na mwaka 2018.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha