

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kushikilia utandawazi wa kiuchumi, ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Ujerumani
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akishiriki semina na wawakilishi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani mjini Berlin, Ujerumani, Juni 19, 2023. (Xinhua/Ding Lin)
BERLIN - Waziri Mkuu wa China Li Qiang Jumatatu ametoa wito kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani kushikilia utandawazi wa kiuchumi na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Ujerumani.
Kampuni zinapaswa kuchukua tena uongozi katika suala la kuzuia hatari, na kuzuia hatari na ushirikiano siyo masuala yanayotofautiana, Waziri Mkuu Li amesema hayo wakati akishiriki semina na wawakilishi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani.
Pia ameonya dhidi ya kufananisha kirahisi tu kutegemeana na hali ya ukosefu wa usalama.
Wawakilishi wa kampuni za Ujerumani zikiwemo Siemens, Volkswagen, Mercedes-Benz, BMW, Schaeffler, BASF, Covestro, Wacker Chemie, Merck, SAP na Allianz walihudhuria semina hiyo.
Kama ilivyopendekezwa na Waziri Mkuu Li, washiriki walikuwa na majadiliano ya wazi na ya dhati pamoja na mazungumzo ya kina juu ya jinsi ya kutazama hali ya sasa ya kiuchumi na kisiasa ya kimataifa, maendeleo ya uchumi wa China, matarajio ya maendeleo ya teknolojia ya siku zijazo, na kile kinachoitwa "kuondoa hatari" na "kupunguza kiwango cha kutegemea" kilichoanzishwa na baadhi ya nchi.
Akibainisha kuwa inaeleweka kuwa pande zote zinafuatilia masuala yao ya kiusalama, Waziri Mkuu Li amesema kilicho muhimu ni jinsi ya kufafanua na kujikinga dhidi ya hatari.
Kama haitashughulikiwa ipasavyo na hali ya hatari ikikuzwa kuliko uhalisia, matatizo zaidi na makubwa yatajitokeza tu, amesema, huku akiongeza kuwa kampuni zina hisia ya moja kwa moja na ya papo kwa hapo kwa hatari na zinajua jinsi ya kuepuka na kukabiliana nayo.
“Kukosa ushirikiano ndiyo hatari kubwa zaidi, na kushindwa kujiendeleza ndiyo ukosefu mkubwa wa usalama,” amebainisha.
Amesema kuwa, pamoja na utandawazi wa kiuchumi, uchumi wa Dunia umeunganishwa, hali ambayo inahusisha mtazamo anuai wa utegemezi.
Waziri Mkuu Li ameelezea matumaini yake kwamba wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili wataweza kufuata mwelekeo uliopo na kuendelea kufuata uwazi, ujumuishaji na ushirikiano wa kunufaishana, na kudumisha uthabiti wa minyororo ya viwanda na ugavi kupitia ushirikiano wa kivitendo wa kiwango cha juu na wa hadhi ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma