Diplomasia ya Rais Xi: Reli ya TAZARA Yashuhudia Urafiki kati ya China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2023

Mwezi Machi, 2013, Xi Jinping aliwasili Tanzania ikiwa ni kituo cha kwanza katika ziara yake barani Afrika baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa China. Ziara yake hiyo ilimfanya Wang Chao asisimka sana, naye ni mfanyakazi wa Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China, wakati huo alikuwa ameanza kufanya kazi kwa nusu mwaka tu katika Tanzania.

Kundi la Uhandisi wa Ujenzi la China analofanya kazi Wang Chao, ambalo hapo awali lilikuwa Ofisi ya Utoaji Msaada kwa nje ya Wizara ya Reli ya China, ilishughulika na uratibu na utekelezaji wa Mradi wa Reli ya TAZARA. Katika wakati huo ambao China haikuwa na fedha nyingi, lakini ilitoa mkopo wa bila riba wa Yuan milioni 988, vifaa na nyenzo zenye uzito wa karibu tani milioni 1, na kutuma watu 56,000 kufanya kazi kwa miaka mitano na miezi minane katika kusaidia watu wa Tanzania na Zambia kukamilisha ujenzi wa Reli ya TAZARA yenye urefu wa kilomita 1,860. Hadi hivi sasa, picha za wakati huo bado zinatundikwa kutani kwenye stesheni ya TAZARA mjini Dar es Salaam, na kila abiria anayefika stesheni hiyo kupanda treni anaweza kuona picha za wafanyakazi wa China na Afrika wakifanya juhudi bega kwa bega kwa ajili ya kujenga reli ya TAZARA .

Stesheni ya TAZARA ya Dar es Salaam. Picha imepigwa na Shen Xiaoxiao.

Stesheni ya TAZARA ya Dar es Salaam. Picha imepigwa na Shen Xiaoxiao.

Jambo linalogusa moyo zaidi ni kuwa, katika wakati wa kujenga reli hii ambayo pia huitwa “njia ya uhuru”, Wachina zaidi ya 60 walifariki. Mnamo Mwaka 2013, Rais Xi aliyekuwa ziarani nchini Tanzania alikwenda kutoa heshima kwenye makaburi ya wataalamu hao wa China waliosaidia Tanzania, ambapo alisema, “majina ya mashujaa hao ni sawa na Reli ya TAZARA yatakumbukwa na watu wa China, Tanzania na Zambia daima milele.”

Katika ziara yake hiyo, Rais Xi kwa mara ya kwanza alifafanua kikamilifu kuhusu dhana ya “kufuata hali halisi, urafiki na udhati” katika uhusiano kati ya China na Afrika. China na Tanzania zilitia saini makubaliano 17 ya ushirikiano wa kirafiki, yaliyohusisha biashara, uwekezaji, ujenzi wa miundombinu, kilimo, mawasiliano ya habari, na kuhuisha maeneo ya utengenezaji wa bidhaa za kuuzwa nje.

Katika miaka 10 iliyopita, Wang Chao alishiriki na kushuhudia ujenzi wa miradi mbalimbali ya kihistoria ya nchi hizo mbili, na cheo chake cha kazi kimepandishwa kutoka fundi hadi msimamizi wa mradi.

Kama alivyofanya Wang, Wachina wa kundi moja baada ya lingine waliotumwa kufanya kazi Tanzania katika miaka ya hivi karibuni, wametumia fursa na kujitolea ujana wao huko, na pia wameshuhudia mabadiliko makubwa yakitokea katika nchi hiyo. Katika muda wa miaka 10 iliyopita, uhusiano kati ya China na Tanzania umeendelea kukua kwa kina, na mioyo ya watu wa nchi hizo mbili imekuwa karibu zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha