Rais Xi Jinping ahimiza watu rafiki kusukuma mbele uimarishaji wa uhusiano kati ya China na Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2023

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping hivi majuzi amejibu barua kutoka kwa mtu rafiki wa Ubelgiji, akimtia moyo kuhimiza urafiki kati ya China na Ubelgiji na China na Ulaya.

Katika barua yake kwa raia huyo wa Ubelgiji, Eric Domb, ambaye ni mkuu na mwanzilishi wa bustani ya wanyama ya Pairi Daiza nchini Ubelgiji, Rais Xi amesema kwamba maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ubelgiji hayawezi kupatikana bila juhudi za muda mrefu na kujitolea bila ubinafsi zilizofanywa na watu rafiki kutoka sekta zote katika nchi hizo mbili.

Ameelezea imani yake kwamba Domb na watu wengine rafiki wataendelea kupanda mbegu ya urafiki, kuvutia watu wengi zaidi, hasa wale wa kizazi kipya, kushiriki kikamilifu katika lengo kuu la urafiki ili kutoa mchango mpya katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Ubelgiji na ule wa China na Ulaya.

“Kujitolea kwa China kwa njia ya maendeleo yenye ubora wa juu yanayotoa kipaumbele kwa uhifadhi wa ikolojia na kuhusisha hali ya maendeleo yaliyo rafiki kwa mazingira na yenye kutoa kaboni chache kutatoa fursa zaidi kwa Dunia na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya binadamu” Rais Xi amesema.

Ameeleza kuwa, kwa sasa, China inahimiza kikamilifu maendeleo ya kisasa ya China ambayo yanahusisha kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili na kutekeleza miradi mikubwa ya uhifadhi wa bioanuwai.

Amesema, idadi kubwa ya viumbe walio hatarini kutoweka wamekuwa chini ya ulinzi mzuri na panda mathalani, wameweza kuondolewa kutoka kwenye kundi la wanyama walio hatarini kutoweka hadi kundi la wanyama wanaohitaji uangalizi wa karibu kutokana na umaalum wao.

Kwenye barua hiyo ambayo Domb alimwandikia Rais Xi hivi majuzi, pamoja na mambo mengine mengi ya kumpongeza yeye binafasi na nchi ya China katika uhifadhi wa mazingira na bioanuai, alikumbuka kwamba Rais Xi na mkewe, Peng Liyuan, walihudhuria hafla ya ufunguzi wa ukumbi mkubwa wa panda kwenye bustani ya wanyama ya Pairi Daiza wakati wa ziara yao nchini Ubelgiji mnamo Machi 2014.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha