

Lugha Nyingine
Wachina wengi zaidi wafanya safari wakati wa Sikukuu ya jadi ya Duanwu iliyoanza jana Juni 22
Abiria wakipanda treni katika Stesheni ya Reli ya Xinchang kwenye reli ya kati ya Hangzhou-Shaoxing-Taizhou katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Juni 19, 2023. (Xinhua/Huang Zongzhi)
BEIJING - Wachina wengi zaidi wamefanya safari katika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Tamasha la Mashua ya Dragoni au sikukuu ya Duanwu iliyoanza jana Juni 22, takwimu rasmi za serikali ya China zimeonyesha Alhamisi.
Takribani safari za barabarani milioni 30.95 zimefanywa Alhamisi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 66.3 mwaka hadi mwaka. Idadi ya safari za majini nchini humo zilikadiriwa kuongezeka kwa asilimia 164.82 kutoka mwaka uliotangulia hadi kufikia milioni 1, Wizara ya Uchukuzi ya China imesema.
Shirika la reli la China linakadiriwa kuhudumia safari milioni 16.2 siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa Shirika la Reli la China.
Safari za reli zinazokadiriwa kufikia milioni 13.86 zimefanywa siku ya Jumatano, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.8 kutoka kipindi kama hicho cha Mwaka 2019.
Sikukuu ya Tamasha la Mashua ya Dragon, ambayo pia huitwa Sikukuu ya Duanwu, huadhimishwa katika siku ya tano ya mwezi wa tano kwa kalenda ya kilimo ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma