

Lugha Nyingine
Tume ya ujengaji wa amani ya Umoja wa Mataifa kukabiliana na uhalifu wa kupangwa katika eneo la Sahel barani Afrika
Tume ya Ujengaji wa Amani ya Umoja wa Mataifa (PBC) imefanya mkutano wa ngazi ya mabalozi kwa lengo la kukabiliana na suala la uhalifu wa kupangwa katika eneo la Sahel barani Afrika.
Akinukuu ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume hiyo Ivan Simonovic kutoka Crotia amesema, hali ya usalama katika eneo la Sahel imeendelea kukabiliwa na mashambulizi yanayofanywa na makundi ya kigaidi na yenye msimamo mkali katika maeneo ya mpakani.
Tume hiyo imekuwa ikijishughulisha kikamilifu katika kuboresha mazingira ya eneo la Sahel, linalojumuisha nchi kadhaa zikiwemo Burkina Faso, Cameroon, Gambia, Mali, na Senegal, na kuunga mkono vipaumbele vya ujengaji wa amani na kusaidia utekelezaji wa Mkakati wa Pande zote wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahel.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu inakadiria kuwa, shughuli haramu za kiuchumi katika eneo la Sahel zimekuwa zikiingiza mabilioni ya dola za kimarekani kila mwaka, huku idadi kubwa ya watu katika eneo hilo wakiishi maisha ya chini ya dola mbili kwa siku.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma