Umoja wa Afrika watoa mafunzo kwa askari polisi wa Somalia kuwasaidia kuboresha ujuzi wa kuongoza magari na usalama barabarani

(CRI Online) Juni 26, 2023

Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ARMIS) imesema imekamilisha mafunzo ya wiki mbili kwa askari 55 wa usalama barabarani wa nchini Somalia ili kuimarisha uwezo wao wa kusimamia usafiri wa magari na kuhakikisha usalama katika barabara za umma.

Tume hiyo imesema mafunzo hayo yaliyomalizika Ijumaa ya wiki iliyopita yalifanyika kwa pamoja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, mji wa Jowhar katika Jimbo la Hirshabelle, Baidoa, katika Jimbo la Kusini Magharibi, na Kismayo katika Jimbo la Jubaland.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, Kamishna wa Jeshi la Polisi la ATMIS Hillary Sao Kanu amewataka askari polisi hao kubadilishana uzoefu waliopata ili kuimarisha utoaji wa huduma hiyo.

Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Somalia Osman Abdullahi Mohamed amesema, mafunzo hayo yatasaidia kubadili usimamizi wa magari katika miji ya nchi hiyo inayokabiliwa na msongamano mkubwa wa magari.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha