

Lugha Nyingine
Waziri mkuu wa China akutana na wakuu wa WTO na WEF
Waziri Mkuu wa China Li Qiang Jumatatu kwa nyakati tofauti amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala na mwenyekiti wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) Klaus Schwab.
Katika mazungumzo na Bi. Okonjo-Iweala, Li Qiang amesema China iko tayari kushirikiana na pande zote kuunga mkono mfumo wa pande nyingi na biashara huria, kupinga mfumo wa upande mmoja na kujihami kibashara, pia kuhimiza mageuzi ya WTO ili kupata maendeleo mapya, na kulinda hadhi ya njia kuu iliyowekwa chini ya mfumo wa biashara wa pande nyingi.
Kwa upande wake, Bi. Okonjo-Iweala amesema WTO inatarajia kujenga uhusiano wa kiwenzi wenye nguvu na China, ili kuchangia katika kuhimiza mageuzi ya shirika hilo na kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi.
Alipokutana na Schwab, Li Qiang amesisitiza kuwa China itashikilia kithabiti njia ya maendeleo ya amani, kufungua mlango zaidi, kushirikiana na pande mbalimbali kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Naye Schwab amesema, WEF iko tayari kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na China, kuhimiza pande mbalimbali kukabiliana kwa pamoja na changamoto mbalimbali duniani ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma