Mkutano wa vyombo vya habari wa Ushirikiano wa eneo la Lancang-Mekong wafanyika Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2023

BEIJING - Mkutano wa Mwaka 2023 wa vyombo vya habari wa Ushirikiano wa eneo la Mto Lancang-Mekong (LMC) unaohusisha nchi sita zikiwemo China, Myanmar, Laos, Thailand, Cambodia, and Vietnam umefanyika Beijing, China siku ya Jumanne.

Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria na kuhutubia mkutano huo.

Zaidi ya wawakilishi 130 kutoka idara husika na vyombo vya habari vya nchi sita hizo za eneo la Lancang-Mekong wamehudhuria mkutano huo. Wamekuwa na mijadala ya kina juu ya kufikia amani na maendeleo, kunufaishana kwa pande zote, na mawasiliano kati ya watu katika kanda hiyo, na juu ya kuchangia ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya Lancang-Mekong inayo karibu zaidi.

Wadau waliohudhuria mkutano huo wamechangia maoni kwamba manufaa halisi yamepatikana kwa nchi hizo sita zinazoshiriki tangu kuanzishwa kwa LMC, na LMC imeongeza urafiki miongoni mwa watu wa nchi hizo sita.

Wamesema, kuna uwezekano mkubwa wa ushirikiano kati ya nchi hizo sita katika maeneo kama vile ujenzi wa miundombinu, kilimo, kupunguza umaskini, usalama na uhifadhi wa mazingira.

Wameelezea matumaini yao ya kukuza mabadilishano kati ya watu wa nchi hizo sita kupitia ushirikiano wa vyombo vya habari, kuimarisha urafiki na hali ya kuaminiana, na kueleza vyema simulizi ya eneo la Lancang-Mekong.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha