

Lugha Nyingine
Mwandishi mashuhuri ahimiza kuongeza maelewano na ushirikiano kati ya China na Marekani
Simon Winchester (People's Daily Online/Liu Ning)
Katika mahojiano ya hivi majuzi na People's Daily Online, mwandishi wa vitabu na mwanazuoni mashuhuri Simon Winchester, ambaye taaluma yake inajumuisha fasihi, historia, teknolojia, na jiografia, ametoa maoni yake kuhusu China na kusisitiza mabadiliko makubwa halisi ambayo ameshuhudia kwa muda mrefu. Amehimiza haja ya kuongeza mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na nchi za Magharibi, na kuitaka Marekani kuimarisha ushirikiano na China.
Simon Winchester (People's Daily Online/Liu Ning)
Mageuzi na maendeleo ya China
Tangu safari yake ya kwanza nchini China Mwaka 1978, Winchester ameona mabadiliko makubwa yaliyotokea nchini China. Amebainisha maendeleo dhahiri yaliyopatikana , hasa katika usafi, ustawi, na usalama. Maendeleo na uboreshaji wa miundombinu, ikiwa ni pamoja na barabara kuu, majengo marefu, na treni za subways, yamemfanya apigwe butwaa.
Mahojiano hayo pia yalihusu kujitokeza kwa China katika sayansi na teknolojia, huku Winchester akikiri kuongoza kwa nchi ya China katika sekta ya viwanda na utengenezaji bidhaa. Ametofautisha kati ya kuvumbua na kuzalisha, na amewahimiza wanasayansi na wavumbuzi wachanga wa China kukubali kuwa na ujasiri bila kuogopa hatari na kuona kushindwa kama sehemu muhimu katika safari yao ya kujifunza.
Kuhimiza mabadilishano ya kitamaduni
Winchester zaidi amewataka watu wa nchi za Magharibi kusafiri hadi China kufanya utafiti juu ya nchi hii kubwa, yenye historia ndefu na ya kuvutia.
Amerejelea kitabu chake cha awali, "The River at the Center of the World," ambacho kinahusu safari yake ya mwaka mzima kote nchini China, akifuata Mto Yangtze kutoka Shanghai hadi Tibet.
Mwandishi huyo amekumbuka kwa uchangamfu mandhari ya kipekee na watu wenye hali mbalimbali aliokutana nao, haswa maeneo ya kusini na magharibi mwa China.
Kutetea maelewano na ushirikiano
Winchester ametoa wito wa kuimarishwa kwa maelewano kati ya China na Marekani, na kusisitiza nguvu bora ya pande hizi mbili katika ushirikiano na kuishi pamoja kwa amani.
"Huawei, kwa mfano, China kwa ujumla, kwa maoni yangu, siyo tishio kwa Marekani," Winchester amesema. Ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa hisia hasi dhidi ya China miongoni mwa wanasiasa fulani wa Marekani, ambazo mara nyingi huonyeshwa katika hotuba zao za hadharani na kuonekana kwenye vyombo vya habari.
Badala yake, anapendekeza kwamba ushirikiano kati ya Marekani na China utakuwa wa manufaa siyo tu kwa nchi hizo mbili bali pia kwa Dunia nzima.
Kuendelea kusoma na kuongeza shauku zaidi
Kuhusu umahiri wake wa kuwa mjuzi wa habari na mambo katika sekta mbalimbali, Winchester amesifu desturi zake nyingi za kusoma na kusafiri mara kwa mara. Ametambua mambo mengi anayopenda na akaona hiyo ni nguvu yake bora katika kuchunguza mada mbalimbali.
Ameonyesha nia yake ya kuendelea kusoma na kusambaza maarifa kupitia maandishi yake.
Amesisitiza udharura wa nchi mbalimbali wa kuondokana na tofauti zao na kushughulikia kwa ushirikiano changamoto na athari zinazoletwa na Teknolojia za Akili Bandia (AI).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma