

Lugha Nyingine
Kenya yaondoa marufuku ya miaka sita ya ukataji miti kwa ajili ya mbao na kuzusha malalamiko kutoka kwa wanamazingira
Serikali ya Kenya imeondoa marufuku ya miaka sita ya ukataji miti kwa ajili ya kupata magogo ya kuzalisha mbao katika misitu ya taifa licha ya wasiwasi wa wanaharakati wa mazingira.
Ingawa Idara ya Misitu ya Kenya (KFS) imesema jamii zinazopakana na misitu hiyo zitanufaika kutokana na uvunaji wa miti uliopangwa, jambo hilo limelalamikiwa na wanamazingira wa Kenya, kwani uamuzi huo umekuja wakati Kenya inakabiliwa na athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi.
Jumapili iliyopita Rais William Ruto alitangaza kuondolewa kwa marufuku hiyo ya ukataji miti, akisema kuna haja ya kuyafungua kiuchumi maeneo yanayotegemea misitu, na kwamba serikali yake imeweka mikakati ya kuhakikisha miti iliyokomaa tu ndiyo inayovunwa, na huku mingine mipya ikipandwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma