

Lugha Nyingine
China yaongeza juhudi za kuleta utulivu kwenye soko la ajira
Mwanafunzi aliyehitimu chuo kikuu akisoma maelezo ya kuajiriwa kwenye maonyesho ya nafasi za kazi katika Wilaya inayojiendesha ya makabila ya Wamiao na Wadong ya Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 30, 2023. (Xinhua/Yang Wenbin)
BEIJING - China imechukua hatua mbalimbali za kuleta utulivu kwenye soko la ajira, kuongeza usaidizi kwa wahitimu wapya wa masomo, nguvukazi ya vijijini, wale walio katika ajira za kunyumbulika na makundi mengine muhimu ya watu wanaotafuta kazi.
Kundi la Kampuni za China International Intellectech limeanzisha kampeni ya kuwezesha ajira kwa wahitimu wapya mwezi huu wa Julai. Shukrani kwa kampeni hii, zaidi ya kampuni 1,300 katika sekta mbalimbali zikiwemo za programu za kompyuta, mambo ya fedha na vifaa vya kielektroniki zimetoa nafasi za ajira zaidi ya 11,000.
Viwanda vya kiserikali vinavyojihusisha na rasilimali watu vimeanzisha ushirikiano na takriban vyuo vikuu 100 ili kufanya shughuli za kipekee za uajiri kwenye maeneo ya vyuo vikuu hivyo katika nusu ya kwanza ya mwaka.
Katika kipindi hicho, kampuni husika pia iliandaa maonyesho 162 ya nafasi za kazi mtandaoni, na kuvutia viwanda na kampuni karibu 41,000 kutangaza nafasi 175,000 za kazi.
Ili kuhimiza kampuni kuajiri vijana wanaotafuta kazi, China imeanzisha sera ya ruzuku kwa kampuni ambazo zinaajiri vijana waliohitimu kutoka vyuo vikuu ndani ya miaka miwili iliyopita, pamoja na vijana wenye umri wa kati ya miaka 16 na 24 ambao wamewasilisha taarifa za kutokuwa na ajira.
Kuanzia mwisho wa mwaka huu, sera hiyo itazipa kampuni ruzuku ya mara moja isiyozidi yuan 1,500 (takriban dola za Kimarekani 208.43) kwa kila mwombaji kazi kijana wanayemwajiri.
Fu Linghui, msemaji wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China amesema,
Hadi kufikia Mwezi Mei, idadi ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 16 na 24 nchini China ilizidi milioni 96, na kati ya hao vijana zaidi ya milioni 33 wameingia kwenye soko la ajira.
Miongoni mwa vijana hao wanaotafuta kazi, vijana zaidi ya milioni 26 wamepata kazi huku wengine milioni 6 bado wakitafuta kazi.
"Uchumi ukiendelea kuimarika, kutakuwa na uungaji mkono madhubuti kwa hali ya soko la ajira kuendelea kuwa tulivu kwa ujumla," msemaji huyo amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma