Rais Xi asisitiza kuweka msingi mpya kwa utayari wa kupigana vita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2023

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu wakati wa ukaguzi wake katika makao makuu ya Kamandi ya Vita ya Mashariki ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) Julai. 6, 2023. Rais Xi, akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa salamu za dhati kwa maofisa na askari wote wa kamandi hiyo. (Xinhua/Li Genge)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu wakati wa ukaguzi wake katika makao makuu ya Kamandi ya Vita ya Mashariki ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) Julai 6, 2023. Rais Xi, akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa salamu za dhati kwa maofisa na askari wote wa kamandi hiyo. (Xinhua/Li Genge)

NANJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesisitiza kufanya juhudi za kutilia maanani malengo ya miaka 100 ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na kuweka msingi mpya wa maendeleo ya kamandi ya vita na utayari wa kupigana vita.

Rais Xi, ameyasema hayo wakati wa ukaguzi katika makao makuu ya Kamandi ya Vita ya Mashariki ya PLA katika Mkoa wa Jiangsu Mashariki mwa China siku ya Alhamisi.

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na Kamati Kuu ya CMC, Rais Xi ametoa salamu za dhati kwa maofisa na askari wote wa kamandi hiyo. Alikutana na wajumbe wao na kupiga picha pamoja nao.

Rais Xi amesifu kwa kutosha mchango mkubwa ambao kamandi hiyo imetoa tangu kuanzishwa kwake katika kulinda mamlaka ya mipaka, haki na maslahi ya baharini ya China pamoja na muungano wa taifa.

“Wakati Dunia ikiingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko, hali isiyo na utulivu na kutokuwa na uhakika inazidi kuonekana katika hali ya usalama wa China ,” Rais Xi amesema.

Ametoa wito wa kuwa macho dhidi ya hatari zinazoweza kutokea na kufanya juhudi za kila upande ili kutimiza jukumu la mapigano ya vita la vikosi vya kamandi za vita.

Rais Xi pia ametoa wito wa kuimarishwa kwa mipango ya vita na mapigano, kuimarisha mfumo wa kamandi kwa ajili ya operesheni za pamoja, na kuongeza mafunzo chini ya hali halisi ya kivita ili kuinua uwezo wa vikosi wa kupigana na kushinda.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na wajumbe wa maofisa na askari wa Kamandi ya Vita ya Mashariki ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na kupiga picha ya pamoja nao wakati wa ukaguzi wake katika makao makuu ya kamandi hiyo Julai 6, 2023. (Xinhua/Li Gang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha