

Lugha Nyingine
Janet Yellen: Kutengana kiuchumi itakuwa balaa kwa Marekani na China
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet L. Yellen Jumapili kwenye mkutano na waandishi wa habari hapa Beijing alisema mazungumzo yake na maofisa waandamizi wa China yalikuwa “moja kwa moja, yenye umuhimu mkubwa, na yenye ufanisi mkubwa”, na amesisitiza kuwa Marekani hailengi kutengana kiuchumi na China, kitendo ambacho “kitakuwa balaa na kuongeza hali isiyo na utulivu kwa nchi hizi mbili na dunia".
Kama ilivyokubaliwa na China na Marekani, Yellen alifanya ziara nchini China kuanzia Julai 6 hadi 9. Alisema, ziara yake hiyo ya Beijing ililenga kuanzisha na kuimarisha uhusiano na viongozi wa kiuchumi wa awamu mpya wa China. Akiongeza kuwa, “Majadiliano yetu ni sehemu ya juhudi kubwa zaidi za pamoja za kuleta utulivu kwenye uhusiano, kupunguza hatari ya kuelewana kwa makosa, na kujadili maeneo ya ushirikiano.”
“Kila upande wetu umeweza kufahamu zaidi kuhusu maamuzi ya kiuchumi na kisera ya upande mwingine, hali ambayo ninaamini ni muhimu sana kwa nchi zetu mbili zilizo zenye uchumi mkubwa zaidi duniani,” amesema Yellen.
Yellen amedhihirisha kuwa, Kutengana kiuchumi kwa nchi hizo zenye uchumi mkubwa zaidi duniani itakuwa balaa kwa nchi zote mbili na kuharibu utulivu wa dunia, na hii karibu haitakuwa na uwezekano wa kufanya hivyo, amesema. “Tunataka kujenga uchumi wa Dunia wenye nguvu na imara ambao ni wazi, huria na wenye haki sawa – na si uliogawanyika au wa kulazimisha nchi kuchagua upande,” amesema.
Yellen amesema, Marekani na China zina maoni yenye tofauti kubwa, “Lakini Rais Biden na mimi sote hatutendei uhusiano kati ya Marekani na China kutokana na migongano kati ya nchi kubwa zenye nguvu.”
“Tunaamini Dunia ni kubwa sana kiasi cha kutosha nchi zetu mbili kustawisha na kupata maendeleo. Nchi zetu mbili zina wajibu wa kusimamia kwa kuwajibika uhusiano huu: kutafuta njia ya kuishi na kunufaika pamoja na ustawi wa Dunia,” ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma