Rais Xi Jinping asisitiza kuwa na uchumi wazi wa kiwango cha juu na kubadilisha muundo wa nishati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 12, 2023

Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne amesisitiza kufanya juhudi za kuweka mifumo mipya ya uchumi ulio wazi wa kiwango cha juu zaidi na kuhimiza mpito wa hatua kwa hatua kutoka kudhibiti matumizi ya nishati kwa kila thamani ya uzalishaji na matumizi ya nishati ya jumla, hadi kudhibiti utoaji hewa ya kaboni kwa kila thamani ya uzalishaji na utoaji wa jumla wa hewa ya kaboni.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), aliyasema hayo alipoongoza mkutano wa Kamati Kuu ya Mageuzi ya Kina ya China ambayo yeye ni mkurugenzi wake.

Amesema kuwa mifumo mipya ya uchumi ulio wazi wa kiwango cha juu ni hatua ya kimkakati ya kuongeza mageuzi na maendeleo kupitia kufungua mlango.

Amesisitiza umuhimu wa kuweka mkazo katika uwazi wa kitaasisi na kuongeza mageuzi ya kitaasisi katika uwekezaji, biashara, mambo ya fedha na uvumbuzi, miongoni mwa maeneo mengine muhimu ya mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa, ili kuinua kikamilifu ufunguaji mlango wa China kwenye kiwango kipya cha juu.

Rais Xi amesema, wakati ikiendelea kujikita na kutilia maanani lengo la kimkakati la kufikia maendeleo ya mambo ya kisasa katika kilimo na maeneo ya vijijini na kujenga nguvu zake katika kilimo, China inapaswa kuchukulia kushughulikia uhusiano kati ya wakulima na ardhi kama kazi yake kuu na kufanya kazi kwa kasi zaidi kuondoa upungufu katika maendeleo ya kilimo na vijiji, ili kuweka msingi imara wa kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika mambo yote.

“Ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia umeingia katika kipindi muhimu ambapo kuondoa utoaji wa hewa ya kaboni imekuwa lengo la kimkakati,” Rais Xi amesema.

Ametoa wito wa kufanya juhudi za kudhibiti matumizi ya nishati hadi kuelekea kudhibiti utoaji wa hewa ya kaboni.

Mkutano huo pia umeeleza kuwa maendeleo ya China yanakabiliwa na hali tata ya kimataifa. Na kwamba juhudi zinapaswa kufanywa ili kuanzisha mfumo mpya wa uchumi ulio wazi wa kiwango cha juu, kuimarisha mageuzi ya kitaasisi katika sekta za biashara na uwekezaji, kupanua ufikiaji wa soko, na kuboresha mazingira ya biashara na huduma na mfumo wa usaidizi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha